Maafisa wa polisi nchini Kenya
wanasema kuwa takriban watu watatu wameuawa katika mji wa kazkazini wa
Wajir, yapata kilomita 100 kutoka mpaka na Somalia.
Watu waliofunika nyuso zao walishambulia duka moja na kufyatua risasi, kulirushia magurunedi kabla ya kulichoma.
Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limeongeza mashambulizi yake kazkazini mashariki mwa Kenya katika siku za hivi karibuni ,na kufanya mashambulizi mawili katika mji wa Mandera ambao una pakana na Somali.
Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa la Somalia la mashambani na limesajili idadi kubwa ya raia Wakenya.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment