Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 18 March 2015

MAKAMU WA RAIS SIERRA-LEONE AFUTWA KAZI

 
 Rais wa Sierra Leone Ernest Koroma kushoto na makamu wake Sam Sumana (Kulia)

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo.

Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia maisha yake.
Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake .
Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana.
Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia.
Hatahivyo amekana madai hayo.
CREDIT: BBCSWAHILI
 

No comments:

Post a Comment