Jengo la kumbukumbu la Tunisia lililolengwa na wapiganaji na kusababisha mauaji ya watu saba
Takriban watalii saba wa kigeni na
raia mmoja wa Tunisia wameuawa baada ya wapiganaji kulenga jengo la
kumbukumbu katika mji mkuu wa Tunisia,runinga ya kitaifa nchini humo
imeripoti.
Kuna habari ambazo hazijathibitisha zilizodai kuwa watu kadhaa wamechukuliwa mateka.
Ufyatulianaji huo wa risasi ulifanyika katika jengo la kumbukumbu la Bardo ambalo liko karibu na bunge katikati ya Tunisia.
Mwanachama mmoja wa bunge aliambia AFP kwamba huduma katika bunge ziliahirishwa baada ya risasi kupigwa na manaibu walikuwa wamekongamana ndani ya jengo hilo.
Msemaji wa wizara wa maswala ya ndani ameiambia Reuters kwamba wanamgambo wawili wamezungukwa ndani ya jengo hilo na vikosi vya usalama.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment