Mkurugenzi wa kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman (kulia) akihutubia wakati uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Bagamoyo, Pwani leo. Wengine kutoka kushoto ni, Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya, Mwenyekiti wa Riadha Tanzania Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende na Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo akisoma hotuba ya mheshimiwa waziri.
Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon yanaandaliwa na kampuni ya 4Beli ya jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti chama cha Riadha Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende (wa pili kushoto) akizungumzia maendeleo ya riadha katika mkoa huo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifawakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon mjini Bagamoyo, Pwani.
CHANZO: HABARIZAJAMII.COM
No comments:
Post a Comment