Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 17 September 2014

WATOTO WAANZA DARASA LA AWALI WAKIWA NA UMRI WA MIAKA 12

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Oldoinyo Sambu wakitafuta huduma za kijamii, ikiwemo maji.

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi wa Kijiji cha Losinoni, Kata ya Oldoinyo Sambu wanalazimika kuanza madarasa ya awali wakiwa na umri wa miaka 12 huku wengine wakishindwa kuhudhuria shuleni kutokana na watoto hao kutembea umbali wa kilometa 40 kwa ajili ya kufuata huduma ya elimu.
Mbali na wanafuzni hao kukabiliwa na changamoto hiyo, wanawake

wa kijiji hicho nao hawahudhurii kliniki kwa ajili ya kupata huduma za mama na mtoto kutokana na kijiji hicho kutokuwa na maeneo ya kujenga zahanati pamoja na huduma nyinginezo za kijamii.
Wakizungumza katika mkutano wa kusikilizwa kero hizo,  wananchi wa kijiji hicho walidai kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa huduma hizo kutokana na kukosekana kwa maeneo kufuatia mwekezaji anayeishi katika kijiji hicho kumiliki maeneo makubwa kinyume na taratibu alizowekewa.
Walidai kuwa hali hiyo ya kutokuwa na maeneo wakati ardhi ipo ya kutosha imewasababishia watoto wao kuanza shule wakiwa na umri mkubwa hali ambayo imekuwa ikiwaletea madhara makubwa ikiwemo watoto hao kukatisha masomo kwa ajili ya mimba na wengine kuolewa kabla ya wakati.
Walisema kuwa mnamo mwaka 2008 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilimuagiza mwekezaji wa shamba la maua la Korovoun Ltd lililopo katika kijiji hicho kuwagawia wakazi wa kijiji hicho kiasi cha ekari 600 kwa ajili ya maeneo muhimu ya kijamii kama kituo cha afya, sekondari, shule ya msingi pamoja na soko lakini mwekezaji huyo alikiuka maagizo hayo.
Mmoja wa wakazi hao Flora Zakayo alisema kuwa akinamama hawahudhurii kliniki mara wapatapo ujauzito kutokana na huduma hiyo kupatikana mbali huku wengine wakijifungulia njiani na wengine kupoteza maisha.
Peter Loisiye, Mwenyekiti wa kijiji hicho alisema kuwa katika ekari 600 zinazomilikiwa na mwekezaji huyo aliwapatia ekari 5 tu kwa ajili ya kujenga shule ya msingi Engadeko ambapo ujenzi huo unaendelea hadi sasa na kwamba eneo hilo ni dogo kwani haliwezi kutosheleza mahitaji ya shule.
Aidha, waliiomba serikali kuingilia kati suala hilo na kuhakikisha kuwa mwekezaji anabakiwa na hekari tano tu huku wao  wakiomba kurejeshewa ekari zilizobaki ili waweze kujenga huduma za msingi zinazowakabili.
Meneja rasilimali watu katika shamba hilo la maua Ismael Ngotee akielezea suala hilo katika mkutano huo alidai kuwa yeye hahusiki na jambo hilo na kwamba haelewi mada alizoitiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment