Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwasalimia
watoto wa wakimbizi wakati Waziri huyo alipokuwa anatembelea baadhi ya
familia za wakimbizi hao kwa lengo la kuwasalimia pamoja na kuangalia
jinsi maisha yao wanavyoyaendesha kambini hapo.
Waziri Chikawe alifanya mkutano na wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani na pia kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Chikawe alifanya mkutano na wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani na pia kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na Wakimbizi wa
Kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kambi hiyo
inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Katika hotuba yake Waziri
Chikawe aliwataka wakimbizi hao kupinga ndoa za utoto ambazo
zinaendelezwa na baadhi ya familia za wakimbizi hao ambapo
inawasababishia watoto hao wa kike kupata matatizo mbalimbali wakati
wanapojifungua. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.


Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto)
akiwasalimia wacheza ngoma ya asili ya nchini Kongo iliyokuwa ikichezwa
na wakimbizi wenye asili hiyo wakati alipokuwa anaingia katika Ukumbi wa
Mikutano uliopo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani
Kigoma kwa ajili ya kuzungumza nao. Waziri Chikawe alifanya mkutano na
baadhi ya wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani pamoja na kupinga ndoa
za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa
inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea zawadi
kutoka kwa Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika kambi
hiyo, aliwataka wakimbizi hao wadumishe amani pamoja na kupinga ndoa za
utotoni ambazo zimeshika kasi katika kambi hiyo kubwa ambayo ina
wahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kushoto kwa Waziri ni Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.



No comments:
Post a Comment