Watanzania
wametakiwa kuwagomea waajiri wanaowalazimisha kuwapima virusi vya
ukimwi kabla ya kuwaajiri kwa sababu wanavunja sheria ya ukimwi ya mwaka
2008 na kanuni yake ya mwaka 2001, inayotilia mkazo haki za kibinadamu
na usiri.
Aidha, sheria hiyo inawakataza waajiri kuwalazimisha wafanyakazi
wao kupima virusi hivyo wakiwa kazini, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuimarisha unyanyapaa ambao ni hatari kuliko virusi vyenyewe.
Wito huo ulitolewa jana na mwenzeshaji wa mafunzo ya ufuatiliaji na uwajibikaji wa jamii katika misingi ya haki za binadamu, Jackson Sikahanga, kwa wajumbe wa kamati za afya, walemavu na watu wanaoishi na VVU kutoka wilaya za Temeke na Ilala, jijini Dar es Salaam.
Akitoa mada kuhusu haki za binadamu, haki ya kupata huduma za afya na haki na wajibu kwa walemavu na wanaoishi na VVU, Sikahanga, alisema haki huwa haiombwi bali inadaiwa na kuwataka wajumbe hao kuhakikisha wanapigania haki zao ikiwamo ya kuishi bila kuwa na wasiwasi.
"Nilichogundua wakati wa mafunzo haya watu wenye VVU na wajumbe wa kamati za afya wengi wao hawana uelewa juu ya sheria ya ukimwi na kanuni yake hivyo kushindwa kudai haki zao ikiwamo ya kupata huduma bora za afya," alisema.
Sikahanga ambaye pia ni mratibu wa shirika la hiyari la Sikika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, alisema ni muhimu watu wakagomea mpango wowote wanaoona ni wa kibaguzi na watambue kuwa kupata huduma za afya ni haki yao kikatiba.
Mratibu wa mafunzo hayo, Jackson Simkoko alisema mradi huo wa mwaka mmoja unaratibiwa kwa pamoja na Chama cha Albino Tanzania (Tas) na asasi ya Community Health Affairs Tanzania (Chat) kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society na una lengo la kuamsha jamii kutambua haki na wajibu katika utoaji na upatikanaji wa afya kwa wote.

CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment