Tamko la Serikali kuhusu uhalali wa bunge maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 15, 2014
Hoja
ya kusitisha bunge maalum la Katiba imehitimishwa rasmi leo na Mahakama
Kuu ya Tanzania iliyoeleza kuwa bunge lipo kisheria na linaweza
kuendelea na kazi zake hadi mwisho wake kisheria.
Waziri
wa Katiba na Sheria ameliambia Bunge Maalum la Katiba
usiku huu kuwa wajumbe 500 sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote 630 wa bunge hilo wanahudhuria bunge wakati wabunge waliosusia bunge ni 130 pekee sawa na asilimia 21 .
usiku huu kuwa wajumbe 500 sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote 630 wa bunge hilo wanahudhuria bunge wakati wabunge waliosusia bunge ni 130 pekee sawa na asilimia 21 .
Amesema
kundi la wajumbe 201 kutoka makundi mbali mbali ya wawakilishi wa jamii
lina wajumbe 189 wanaoshiriki bungeni Kati ya 500 wanaohudhuria bunge
hilo.
Amefafanua kuwa
wajumbe 348 wanaohudhuria bunge la katiba linaloendelea wanatoka
Tanzania Bara Kati yake 125 wanatoka kundi la 201 na kwa wajumbe
wanaotoka Zanzibar wapo 152 ambapo Kati yake 64 ni wa kundi la 201
wanahudhuria bunge la Katiba.
Mheshimiwa
Migiro amesema bunge linaloendelea hivi sasa lina wawakilishi wanaotoka
vyama 18 vya siasa nchini wakati vyama vilivyosusia bunge hilo ni 3 vya
Chadema, CUF na NCCR Mageuzi .
Amefafanua
kuwa wajumbe waliosusia bunge Maalum la katiba hawafiki theluthi moja
ya wajumbe wote hivyo wajumbe walio wengi wanaweza kutumia wingi wao na
uhalali wa kisheria na kisiasa kuendelea na majukumu yao hadi Oktoba 4
litakapokoma kisheria.
Amesema
wito unaotolewa na baadhi ya viongozi wa kulazimisha kusitisha bunge
hilo sio sahihi. Taifa halina mgogoro wa kisiasa. Hakuna sababu ya
kuruhusu Watu kujazwa hofu.
"
Serikali ipo macho na itasimamia Sheria na taratibu zilizowekwa ili
kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za kutafuta riziki na
mchakato huu uliopo kisheria unaendelea kwa amani" amesema Dr Migiro

No comments:
Post a Comment