Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kutaka Bunge Maalumu lifikie ukomo Oktoba 4, mwaka huu yamezua sintofahamu mjini hapa huku uamuzi huo ukionekana kuwachanganya viongozi wa Bunge hilo.
Kutwa nzima ya
jana, viongozi wa Bunge Maalumu walishinda kwenye vikao vya mashauriano
huku wabunge wa CCM wakitarajiwa kukutana jana usiku kwenye makao
makuu ya chama hicho kupewa taarifa rasmi za uamuzi huo.
Katika
makubaliano baina ya TCD na Rais Kikwete, imeamuliwa kuwa uamuzi wa
Rais kupitia Tangazo la Serikali (GN) 254 la kuongeza siku 60 hadi
Oktoba 4 uheshimiwe na baada ya tarehe hiyo Bunge liahirishwe.
Uamuzi
huo ni kinyume cha azimio la Bunge Maalumu la Agosti 5, 2014 ambalo
lilirekebisha Kanuni ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku
zilizotajwa kuwa za kazi, pia sikukuu na siku za Jumapili.
Mwenyekiti
wa Bunge, Samuel Sitta alikaririwa akiwaambia wajumbe wa Bunge hilo
kwamba Rais alikuwa ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazingejumuisha
Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.
Ni kwa msingi
huo, Bunge hilo likapanga kwamba lingeendelea na shughuli zake hadi
Oktoba 31, wakati Mwenyekiti wa Bunge atakapokabidhi Katiba
inayopendekezwa kwa Rais Kikwete.
Hata hivyo,
makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa TCD na Rais yanaonekana
kuvuruga kabisa ratiba ya Bunge hilo ambalo jana na juzi, Kamati ya
Uongozi ilikutana mara kadhaa kuona jinsi ya kunusuru mchakato huo.
Ingawa
haikufahamika mara moja kama vikao hivyo vya kamati ya uongozi
inayoongozwa na Sitta mwenyewe vinajadili nini, lakini taarifa zimedai
huenda kukawa na mabadiliko makubwa ya ratiba.
Habari
nyingine zinadai kwamba mabadiliko hayo huenda yakapunguza muda wa
baadhi ya shughuli za kazi za Bunge hilo ili liweze kukamilisha kazi
yake ikiwamo wajumbe kupiga kura ya uamuzi.
Katika
kikao cha jana asubuhi, kamati hiyo ilishindwa kurekebisha ratiba yake
ili iendane na siku zilizosalia, hivyo kuahirishwa kwa kuwapa kazi
wataalamu wake kuleta mapendekezo ambayo yangejadiliwa jana mchana.
Katibu
wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha jana kwamba ratiba
ya Bunge imebadilika kutokana na hoja nyingi kukubalika ndani ya
kamati.
“Kamati ya uongozi itakutana baadaye (jana)
kuangalia vipengele ambavyo hawakukubaliana kwenye kamati ndivyo
wavipangie muda na ratiba itajulikana baada ya kikao hicho,” alisema
Hamad.
Hofu ya akidi
Taarifa ya TCD
Hofu ya akidi
Hata hivyo,
habari zaidi zinadai kwamba uongozi wa Bunge Maalumu ulichanganywa na
kuwapo kwa hoja za baadhi ya wajumbe wake kutaka kwenda Makka kwa ajili
ya kushiriki Ibada ya Hijja, hali inayotishia akidi kwa ajili ya
kuendesha vikao.
Kanuni za Bunge Maalumu zinataka
kuwapo kwa nusu ya wajumbe kutoka pande zote za Muungano wakati wa
kuendesha vikao vyake na theluthi mbili ya wajumbe hao kila upande
wakati wa kufanya uamuzi au kupiga kura.
“Tumetoka
kwenye kikao mchana huu na pengine tutaitana tena maana hatujafikia
mwafaka, kuna mambo mengi yamejitokeza lakini kubwa ni hili la wenzetu
ambao wanataka kwenda Hijja, kuondoka kwao kunaweza kuathiri akidi kwa
kiasi kikubwa,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo.
Kutokana
na matakwa hayo, hivi sasa Ofisi ya Katibu wa Bunge inafanya tathmini
ili kufahamu idadi ya wajumbe ambao watakwenda Hijja Septemba 22, mwaka
huu, ambao wengi wanatoka Zanzibar.
Hamad alikiri
kwamba kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inayafanyia kazi na kwamba
hilo la Hijja ni mojawapo... “Kwa sasa siko katika nafasi ya kuzungumza
kwa kirefu, kikao cha Kamati ya Uongozi kimeisha na bado kuna kazi
nyingi za kuona jinsi tunavyoendelea.”
Tayari Bunge
hilo limetikiswa na kutokuwapo kwa wajumbe waliosusia vikao tangu
Aprili 16, mwaka huu ambao ni wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR
Mageuzi na baadhi kutoka Kundi la 201.
Taarifa ya TCD
Jana
saa 7:00 mchana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alikutana na wanahabari
na kueleza kuwa katika mazungumzo yao na Rais wamekubaliana mambo
matano ya msingi kwa mustakabali wa nchi.
Alisema
pamoja na kazi ya msingi iliyofanywa na Bunge Maalumu, mchakato
unaoendelea hauwezi kutoa Katiba Mpya ambayo itatumika katika Uchaguzi
Mkuu wa 2015.
“Muda hautoshi kukamilisha mchakato na
kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya sheria, kanuni na taasisi
mbalimbali zinazohitajika,” alisema Cheyo ambaye pia ni Mbunge wa
Bariadi Mashariki (UDP).
Alisema kura ya maoni
ilipangwa kufanyika Aprili 2015 na kama itabidi irudiwe, basi itabidi
irudiwe itakuwa Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la Jamhuri
linatakiwa livunjwe.
Bunge Maalumu
Mabadiliko ya 15 ya Katiba
“Ili Katiba Mpya itumike katika Uchaguzi
Mkuu wa 2015, itabidi uhai wa Bunge na Serikali uongezwe zaidi ya
2015, jambo ambalo sisi viongozi wote hatuliungi mkono,” alisema Cheyo.
Alisema
kwa kutambua kuwa kama kura ya maoni ikifanyika, italazimisha Uchaguzi
Mkuu wa 2015 kuahirishwa, wamekubaliana kura hiyo iahirishwe hadi
baada ya uchaguzi huo.
Bunge Maalumu
Cheyo
alisema Bunge Maalumu kwa sasa linafanya kazi kwa mujibu wa Tangazo la
Serikali (GN), namba 254 lililotolewa na Rais Kikwete ambalo uhai wake
utakoma Oktoba 4.
“Inategemewa kuwa Oktoba 4 Katiba
inayopendekezwa itapatikana. Tulikubaliana hatua hii iachwe ifikiwe na
baada ya hapo Bunge liahirishwe hadi baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
“Tarehe
4 Oktoba ndiyo mwisho. Hiyo ndiyo sheria iliyopo, sisi hatuna mamlaka
ya kuandika GN mpya, GN imetolewa na Bunge hili liko kihalali.
Tulichokuwa tunabishana lisife kesho,” alisema.
Akijibu
maswali ya wanahabari kama ana uhakika Bunge hilo litaweza kukamilisha
kazi yake ndani ya siku zilizobaki, Cheyo alisema “Tumeheshimu sheria
iliyopo tarehe nne Watanzania wanategemea Katiba Mpya itakuwa
imepatikana, sasa kama haitapatikana hilo msiniulize kwa sababu hilo si
jukumu langu.”
Alipoulizwa kama rais ajaye baada ya
Uchaguzi Mkuu wa 2015 ataendeleza mchakato pale ulipoishia alisema:
“Naomba Mungu rais ajaye awe anayejali maoni ya wananchi hilo naomba
kabisa. Sasa tukipata rais ambaye hatutambui sisi wote na mawazo yetu,
basi tutakuwa tumekosea katika kupiga kura.”
Mabadiliko ya 15 ya Katiba
Cheyo
alisema kwa vile Uchaguzi Mkuu wa 2015 utafanyika kwa kutumia Katiba
ya 1977, ni vyema yakafanyika mabadiliko madogo ili kuruhusu uchaguzi
huru na wa haki.
Mabadiliko hayo yatalenga kuwezesha
uwapo wa tume huru ya uchaguzi, mshindi wa urais ashinde kwa zaidi ya
asilimia 50, kuruhusu mgombea binafsi na kuingiza ibara itakayoruhusu
matokeo ya urais kupingwa mahakamani.
“Vyama vya
siasa ambavyo vinapenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika
Katiba ya 1977 vinaombwa kufanya hivyo kwa vile muda tulionao ni
mdogo,” alisema Cheyo.
Ukawa kurudi bungeni
Alisema walikubaliana kuwa marekebisho
hayo yafanyike katika Bunge la Jamhuri litakaloanza Novemba 5 na
ikishindikana yafanywe Februari 2015.
Ukawa kurudi bungeni
Cheyo
alisema suala la kurudi au kutorudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba
kwa wajumbe wa Ukawa halikuwa sehemu ya mkutano kati ya Rais na TCD.
“Kila
siku nasema uamuzi wa vyama tuuheshimu. Wale wana sababu zao za
kutoingia bungeni ni lazima tuheshimu msimamo wao kwa sababu wanazo
sababu,” alisema.
CREDIT: MWANANCHI
CREDIT: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment