Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 11 September 2014

PASCHAL KATAMBI PATROBAS NDIYE MWENYEKITI MPYA WA BAVICHA

Paschal Katambi Patrobas akiwa nchini Ujerumani kuwakilisha Bavicha

Licha kumpigia mizengwe mingi kupitia mitandao ya kijamii kwamba ni mamluki, hatimaye Pachal Katambi Patrobas amechaguliwa kwa kura 173 kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).
Katika uchaguzi uliofanyika jana, Patrobas alimshinda mpinzani wake Upendo aliyepata kura 70, hivyo kuwafunga midomo waliokuwa wakisamabaza taarifa kwamba hastahili kuwania nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo za mitandao, ilidaiwa kwamba Patrobas, ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya Sahara Media Group Limited kama Mwanasheria, ati alipewa fedha za Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Mwandu Diallo, ambaye ndiye mwajiri wake, tuhuma ambazo hazikuweza kuthibitishwa.
Aidha, ilielezwa kwamba baada ya kunyimwa ruhusa ya kwenda Dar es Salaam kwenye uchaguzi, Dk. Diallo aliingilia kati na kumpatia ruhusa hiyo, huku taarifa zikisema hata tikiti ya ndege alifanyiwa booking na katibu wa Diallo.
Lakini hatimaye uchaguzi huo ulifanyika kwa utulivu mkubwa na matokeo ya wajumbe walioshinda ni haya hapa:

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA
1 JAPHET ELIBARIKI MOSHI
2 EDSON JOEL MWEMAELU
3 MASULE SAMSON MASAGA
4 PENINA ERNEST NKYA
5 DANIEL EZEKIEL MSWELO
6 LUTGAR CHEMICHA HAULE
7 ELIZABETH JOSEPH RIZIKI
8 SAMWEL GIBSON SHAMI
WAJUMBE MKUTANO MKUU (ZANZIBAR):
1. ALLY KASSIM ISMAIL
2 SUED RKADHIR ABDULAHIMID
3 HASSAN ABDALAH HAMIS
WAJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA (BARA)
1 PASQUINA FERDINAND LUCAS
2 PAMELA SIMON MAASAY
3 JOSEPH LOTH KASAMBALA
4 HELLEN NANGUSU DALALI
MAKAMU M/KITI WA BAVICHA TAIFA (ZANZIBAR)
• ZEUDI MVANO ABDULAHI
MAKAMU M/KITI WA BAVICHA TAIFA (BARA)
• PATRICK SOSOPI KAPURA
MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA
• PASCHAL KATAMBI PATROBAS

No comments:

Post a Comment