Mwalimu wa Shule ya Msingi Makurumla, Maria Samuel Hoza akiwa katika harakati za kufunga ndoa yake ya pili.
MWALIMU mmoja
wa Shule ya Msingi Makurumla iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam,
Maria Samuel Hoza, amejikuta akiaibika vibaya baada ya mumewe, Bryton
Muhanje kumkuta akiwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa nyingine
kwenye Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga, Jumamosi iliyopita.
Gazeti
hili lilimshuhudia Muhanje, akiingia kanisani na kwenda moja kwa moja
mbele ya altare na kumzuia Padri Richard, ambaye alikuwa amemaliza
kufungisha ndoa ya kwanza, asifanye hivyo kwa maharusi wanaofuata kwa
vile ni batili.
Chanzo
chetu makini cha habari kililidokeza gazeti hili juu ya kuwepo kwa
mpango wa mwanamke ambaye yupo katika ndoa, kutaka kuolewa tena na mtu
mwingine bila mumewe kujua. Kufuatia ‘tip’ hiyo, kikosi kabambe cha
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilifanikiwa kupata namba ya mwanaume huyo
na kufanya naye mawasiliano ili kujua ukweli wa madai hayo.
Mume wa Maria Samuel Hoza, Bryton Muhanje (kulia) akitoa pingamizi la ndoa ndani ya Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga.
Muhanje
alikiri kupata tetesi hizo, lakini alikuwa akihaha kujua sehemu
itakakofanyika harusi hiyo na kwamba timu ya vijana wake ilijipanga
kuhakikisha anafahamu eneo hilo.Baadaye aliwaeleza OFM kuwa alikuwa
alisikia ndoa hiyo ingefungwa Magomeni, hivyo alikodi pikipiki sita
zilizofanya doria katika makanisa yote yaliyopo eneo hilo ili kujua
mkewe alikuwa kanisa gani.
Pamoja
na hivyo, mwanaume huyo pia alikwenda hadi shule anayofundisha mwalimu
huyo na kwa kuwa hawamfahamu, alijitambulisha kama ndugu yake na kwamba
alikuwa anaomba kujua kanisa ambalo (mkewe) atafunga ndoa, kwani
ameelezwa kuwa lipo Magomeni lakini hakuelewa ni lipi.
“Wanafunzi
wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga,
ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo,
nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye
harusi hiyo,” alisema.
Padri Richard akitoka nje ya kanisa hilo mara baada ya pingamizi la harusi kutokea.
OFM
ikiwa tayari kwa kunasa tukio hilo, walikuwa wameshatinga kanisani hapo
mapema na kushuhudia maharusi watatu tofauti wakijiandaa kufunga ndoa,
wakiwemo Maria na mwenzake.
Ratiba
ilionyesha kwamba ndoa ya wawili hao ilikuwa ya pili, hivyo mara tu
zamu yao ilipofika na Padri Richard kuanza kutoa risala ya kuwapongeza
kwa hatua waliyofikia, wote walionekana kuwa na bashasha ya siku hiyo
muhimu ya kuungana.
Ghafla
bila kutarajia, wakati wasaidizi wa padri wakimletea kibakuli chenye
pete ya ndoa, Muhanje alijitokeza na kumuomba mchunga kondoo huyo
kusitisha zoezi hilo kwa vile anayetaka kufunga ndoa, ni mke wake
halali.
Makamanda wa Polisi wakiwa nje ya kanisa tayari ili kutuliza ugomvi.
Akiwa
amepigwa na butwaa, padri huyo alilazimkika kwanza kumuuliza bibi
harusi kama anamtambua mtu aliyesimama mbele yake, lakini akiwa mkavu
alikataa akidai hajawahi kumuona maishani mwake.
Mume
akiwa ameongozana na mpambe wake aliyesimamia ndoa yake, alimuomba
padri atoe vielelezo kuthibitisha ukweli huo na baada ya kupewa nafasi
hiyo, alionesha picha mbalimbali za siku ya harusi yao, nakala ya cheti
cha ndoa na akaomba pia aruhusiwe atoe kompyuta yake mpakato ili
achezeshe video ya siku hiyo ya Oktoba 29, 2009 alipofunga naye ndoa
katika Kanisa la KKT Kimara Korogwe, Dar.
Kwa
ushahidi huo, padri huyo alikubaliana naye na kusimamisha zoezi hilo na
kuwataka kuongozana kwenda ofisini kwa mazungumzo zaidi. Baada ya
mazungumzo marefu ofisini, padri huyo alikubaliana na hoja za mume na
hivyo kusitisha zoezi hilo, akidai mwanamke huyo hawezi kuolewa kwa mara
ya pili.
Ilifahamika
baadaye kuwa Maria, ambaye amezaa mtoto mmoja na Muhanje, alitumia jina
la Neema Stanley Hoza katika kusudio lake la kufunga ndoa ya pili.
Baadhi ya wapambe na wanandugu wakirudi makwao mara baada ya ndoa kubatilishwa.
Hata
hivyo, wakati kukiwa na sintofahamu ya tukio hilo kanisani, ghafla
kikosi cha askari polisi wakiwa katika ‘difenda’ kilitia timu
kuhakikisha usalama unakuwepo.Askari hao walisema walipewa taarifa za
kuwepo kwa tukio ambalo lingeweza kuhatarisha amani na ili kuhakikisha
jambo hilo linatokea, waliondoka na maharusi wa pili baada ya taratibu
za kikanisa kukamilika.
Baada
ya tukio hilo, Muhanje alisema alimuoa mkewe mwaka huo, baada ya kuwa
ameishi naye kinyumba kuanzia mwaka 2005.“Baada ya kukaa naye kwa miaka
minne, tukaamua kufunga ndoa mwaka huo wa 2009 na baada ya hapo, yeye
akaenda kufanya kazi ya ualimu Lushoto katika Shule ya Shambalai.
Picha ya ushahidi ikionesha ndoa ya halali kati ya Bw. Bryton Muhanje na Mwl. Maria Samuel Hoza.
“Mwanzo
tulikuwa na maisha mazuri tu na katika kipindi hicho, nilijitahidi
kumfanyia utaratibu wa uhamisho ili aje Dar na kufanikiwa kumleta mwaka
2012 na alipangiwa Shule ya Makurumla.“Baadaye kidogo hali yangu kifedha
ikayumba, ndipo matatizo yalipoanza kwani kitendo cha kutegemea hela za
mshahara wake katika maisha kikamshinda, akaanza kutafuta visa
mbalimbali ili mradi mimi nimpige apate sababu ya kuondoka.
“Alifanya
vituko vingi sana, wakati mwingine alifunga mlango na kuondoka na
funguo na kwenda kwa dada yake na kulala huko huko, wakati mwingine
aliamua tu kuvunja vitu bila kujali hadi mwaka jana mwezi wa nne
alipoondoka moja kwa moja kwenda kusikojulikana.“Siku chache zilizopita
ndipo nilipopata habari kwamba ana mpango wa kuolewa, ndipo nikaanza
kufuatilia ili nijue.
“Nilipokuwa
pale kanisani wakati wa kuzuia ndoa, yule mwanaume aliyetaka kumuona
mke wangu, alinitishia kuwa atanikomesha, nimeenda polisi kuripoti maana
siwezi kujua atafanya nini na nimefungua jalada lenye namba
MAG/RB/8452/2014 KUTISHIWA KUUA KWA MANENO.”
CREDIT: GAZETI LA UWAZI
No comments:
Post a Comment