Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 3 September 2014

MSICHANA AUAWA AKIMTETEA BABA YAKE

Unyanyapaa dhidi ya wanawake ni jinamizi kubwa India
Polisi nchini India wanasema kuwa msichana mmoja ambaye alijaribu kumtetea babake kwenye baraza moja la kijiji amepatikana akiwa amekufa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 na babake waliitwa na wazee wa kijiji katika eneo la Bengal Magharibi kutatua mzozo kuhusu tingatinga.
Palisi wanasema kuwa huenda msichana huyo alibakwa kabla ya kuuawa kwani mwili wake ulipatikana ukiwa uchi. Inaarifiwa msichana huyo alikejeliwa na wanakijiji kwenye baraza hilo kwa kuteta ambavyo babake alidhulumiwa.Inaripotiwa kuwa msichana huyo alipinga ambavyo babake alitendewa alipodhulumiwa na kisha kutoweka
Familia ya msichana huyo inasema kuwa alilazimishwa kutema mate ardhini na kuyaramba mate hayo, kitendo kinachoonekana kuwa cha unyama sana.
Mahakama zisizo rasmi nchini India hutoa adhabu dhidi ya wanakijiji wanaoonekana kuvunja sheria za kijiji kile.
Vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake nchini India vimeanza kumulikwa tangu ubakaji wa mwanafunzi mmoja mwaka 2012 kwenye basi la abiria.

Serikali ilidhibiti sheria za ubakaji mwaka jana baada ya maandamano makubwa kufuatia shambulizi hilo lakini unyanyapa dhidi ya wanawake bado ni janamizi.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment