Baadhi
ya majimbo ya uchaguzi ya Zanzibar yapo hatarini kupunguzwa kutokana na
kuwa na idadi ndogo ya wananchi. Miongoni mwa majimbo hayo, ni Mgogoni,
kisiwani Pemba, ambalo mwakilishi wake ni Waziri wa Katiba na Sheria
Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari (CUF).
Hali hiyo imedhihirika baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kukusanya maoni kwa hatua ya awali kutoka kwa wananchi mbalimbali ingawa bado haijafanya maamuzi ya ugawaji wa majimbo.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salum Jecha, alisema tume ilianza kukusanya maoni Juni 9, mwaka huu, kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya majina, idadi na mipaka ya majimbo ya uchaguzi na kwamba, kazi hiyo kwa awamu ya mwanzo imekamilika.
Alisema maoni makuu waliyopokea kutoka kwa wadau, wakiwamo wananchi, asasi za kiraia, asasi za kiserikali na wanasiasa, yalihusu matatizo ya mipaka ya majimbo kwa wilaya, wadi, shehia, ongezeko la idadi ya watu katika majimbo na tatizo la mgawanyo wa majimbo kijiografia.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Zec imepewa mamlaka ya kugawa majimbo ama kuongeza kufikia majimbo 55 au kupunguza kufikia majimbo 40 kutokana na idadi ya watu.
“Yapo baadhi ya majimbo yana idadi kubwa ya wakaazi na yanastahili kukatwa na kuwa majimbo mawili tofauti na majimbo mengine yana idadi ndogo ya wakaazi, yanastahili kukatwa mfano majimbo mawili kufanywa jimbo moja tu ”alisema Jecha.
Akizungumzia baadhi ya majimbo, ambayo yana idadi kubwa ya wananchi, Mkurugenzi wa Zec, Salum Kassim Ali, alisema jimbo la Dimani, ambalo lina wakaazi zaidi ya 58,000, Fuoni zaidi ya 65,000 na Dole zaidi ya 39,000.
Majimbo yenye idadi ndogo ya wananchi, ni Mgogoni, ambalo lina wakaazi 17,000, Chambani 15,000 na Rahaleo 16,000.
Jimbo la Mgogoni na Chambani ni miongoni mwa majimbo 18 kisiwani Pemba, ambayo yote yanaongozwa na Chama cha Wananchi (CUF).
Alisema changamoto, ambazo wamekumbana nazo katika ukusanyaji wa maoni hayo kwa hatua ya awali, ni baadhi ya watu kuwa na jazba za kisiasa na uhaba wa fedha na kwamba, matatizo hayo walikabiliana nayo.
Salum alisema mchakato mzima wa ukusanyaji maoni wa Zec utakamilika Machi 2015 na kwamba, Zec ndipo itakapotoa maamuzi ama ya kupunguza au kuongeza majimbo kutokana na maoni ya walio wengi waliyowasilisha.
Jumla ya Sh. milioni 422 zinatarajiwa kutumika katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni kuhusu mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi Zanzibar.
Mara ya mwisho Zec iligawa majimbo mwaka 2002 na kwamba, Pemba majimbo yalipunguzwa kutoka 21 hadi 18 na Unguja kuongezwa kutoka 28 hadi 32 na kufanya Zanzibar kuwa na majimbo jumla 50.

No comments:
Post a Comment