RPC Suleiman Kova
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
02/09/2014
GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE LAKAMATWA NA VIPANDE 70 VYA NONDO MALI YA WIZI NA WATUHUMIWA SITA
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam limekamata gari namba T 784 AFA, Toyota HIACE likiwa na vipande 70 vya Nondo. Gari hili limekamatwa tarehe 29/08/2014, majira ya saa saba usiku maeneo ya barabara ya Ferry Kimbiji baada ya askari waliokuwa doria kupokea taarifa kuwepo kwa gari hilo lililobeba mali hizo idhaniwayo kuwa ni ya wizi.
Aidha taarifa za awali zinaonyesha kuwa mali hiyo imeibwa katika maeneo mbalimbali ya ujenzi unaoendelea huko maeneo ya Kimbiji na Somangira Kigamboni Mkoa wa Kipolisi Temeke.
Watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1. SHIJA S/O MGENI, Miaka 22, Mkazi wa Mbagala
2. ALLY S/O MANGILUNGI, Miaka 18, Mkazi wa Kurasini.
3. NASSORO S/O RAMADHANI, Miaka 35, Mkazi wa Mbagala Charambe.
4. RAJABU S/O HASSAN, Miaka 32, Mkazi wa Mbagala Charambe.
5. SAMSON S/O MDINGI, Miaka 27, Mkazi wa Kurasini.
6. AMINI S/O SAID, Miaka 15, Mkazi wa Kurasini.
Nawaomba wananchi waendelee kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhakika zitakazosaidia kuwakamata wahalifu kama hawa wanaodhoofisha jitihada za maendeleo kwa wawekezaji na Serikali kwa kupora vifaa vya miundombinu ya ujenzi na vitu kama hivi.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment