Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 10 September 2014

KIAMA KIMEKARIBIA: TAZAMA WACHUNGAJI WANAVYOFANYA UTAPELI KWA NENO LA MUNGU

Ndugu zangu,
Maneno ya Manabii waliotajwa kwenye Vitabu Vitakatifu sasa yanatimia. Wachungaji wa Kondoo wa Mungu hivi sasa wanachezea kamari maneno matakatifu ili kutimiza nia na dhamira ya utapeli wao.
Tumesikia mara kadhaa vitendo visivyofaa vya viongozi wa dini katika jamii - ubakaji, ujambazi, uzinzi na sasa utapeli wa kutisha kwa kujifanya wanafanya miujiza wakati siyo kweli. Wengine wanafikia hatua ya kusema kwamba wanafufua wafu, lakini ukiangalia kwa undani utagundua kwamba wale wanaodaiwa kwamba wamefufuliwa, kumbe ni 'watu wa kupanga' tu na wachungaji hao ili kuongeza idadi ya waumini kanisani na hivyo kuongeza ndururu zao kwenye vikapu vya sadaka.
Haya yanatokea hapa Tanzania na wengi ni mashahidi. Hata hivyo, video hii inadhihirisha kwamba vitendo hivi vimezagaa kila sehemu Afrika, ikiwemo nchi jirani ya Kenya ambapo mchungaji huyu kwanza amefanya uzinzi na kahaba, halafu akatumia hila kumtaka ajifanye mlemavu halafu yeye amponye.
Tutafakari tunakoelekea, manabii wa uongo ni wengi sana. Shika sana ulicho nacho, asije muovu akakupotosha!
Mungu ni Yule jana leo na hata milele!

Ndugu yenu,
Daniel Mbega.

No comments:

Post a Comment