


Karibu watu 15 wamekufa na mamia wengine bado wamefukiwa baada ya Kanisa la mhubiri TB Joshua kuporomoka jana Ijumaa.
Kanisa hilo - Synagogue Church of All Nations (SCOAN) lililoko
Ikotun, Lagos lenye ghorofa sita - lilibomoka jana majira ya saa 7 mchana (saa 10 kwa Saa za Afrika Mashariki).
Ikotun, Lagos lenye ghorofa sita - lilibomoka jana majira ya saa 7 mchana (saa 10 kwa Saa za Afrika Mashariki).
Msemaji wa Mamlaka ya Huduma ya Dharura katika Jimbo la Lagos, Friday Adeboayo, alithibitisha kwamba miili ya watu 15 iliopolewa kwenye kifusi.
Inaelezwa kwamba, vyombo ya habari vilizuiliwa kukaribia eneo la tukio.
TB Joshua, maarufu kama "Nabii", ni miongoni mwa wahubiri maarufu wa Nigeria akiwa na maelfu ya wafuasi ulimwenguni kutokana na miujiza yake anayoifanya pamoja na utabiri.
Kanisa hilo, ambalo hutumiwa kama nyumba ya kulala wageni wa ndani na kimataifa, hutembelewa na maelfu ya watu kila mwaka.“Watu wanatoka kila sehemu duniani kushuhudia na kupokea miujiza ya Mungu kupitia maisha ya Nabii TB Joshua,” ndio ujumbe ulioandikwa kanisani hapo.
Katika maendeleo mengine, Wakala wa Taifa wa Huduma za Dharura (NEMA) umetoa taarifa kuhusiana na jengo hilo lililoporomoka.
Msemaji wa NEMA, Ibrahim Farinloye, alisema kwamba jengo hilo awali lilipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini katika mshangao wa wengi, zikajengwa ghorofa tano.
“Hizo nyingine tatu zilikuwa zinaendelea kujengwa wakati jengo lilipoporomoka saa 7 mchana (Saa 10 alasiri) wa Ijumaa.
“Washirika wa kanisa hilo walikuwa wakali na wakataka kuwashambulia wafanyakazi wa mamlaka waliokwenda kwa ajili ya uokoaji.
“Kabla ya kuwasili kwa waokoaji hao, karibu watu 15 walikuwa wameopolewa wakiwa hai na watatu wakiwa wamekufa. Waokoaji wameokoa watu watatu wakiwa hai na maiti tatu, lakini kuna watu wengi ndani,” alisema Farinloye kupitia kwenye ujumbe wa sms.
No comments:
Post a Comment