Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 13 September 2014

HALIMA MDEE MWENYEKITI MPYA BAWACHA

Mhe. Halima James Mdee

 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah. 

Mbunge wa Kawe Halima James Mdee ndiye Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) licha ya kelele za baadhi ya watu kwamba yeye ni msichana tu, hajaolewa na kwamba hakustahili kuwaongoza wanawake wa chama hicho.
Katika uchaguzi uliomalizika jana usiku Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mdee aliibuka mshindi kwa kuzoa kura 165 kati ya 244 zilizopigwa huku aliyemfuatia kwa karibu, Janeth Rith akipata kura 35.
Wapinzani wake wengine, Sophia Mwakagenda alipata kura 18, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Chiku Afla Abwao alipata 15 na Lilian Wassira aliambulia kura 11.
Nafasi hiyo iliachwa wazi na Mbunge wa Viti Maalum Suzan Lyimo ambaye sasa amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema.
Makamu Mwenyekiti wa Bawacha Zanzibar, aliyeibuka mshindi ni Amida Abdalah ambaye alipata kura 194, akifuatiwa na Maria Msabaha aliyeambulia kura 36.
Kwa upande wa Bara, Hawa Mwaifunge alishinda nafasi hiyo kwa kura 136 akifuatiwa na Victoria Benedict kwa kura 96.
Kamati Kuu itakaa leo kuandaa ajenda za kikao cha Baraza Kuu, kabla ya kuitisha Mkutano Mkuu wa chama, utakaofanyika kesho kumchagua Mwenyekiti wa Taifa na Makamu wake kwa Zanzibar na Bara.
Septemba 15, Baraza Kuu litakutana kuchagua Katibu na makamu wake wa Tanzania Bara na Zanzibar na wajumbe wa Kamati Kuu na Septemba 16 Kamati Kuu ya chama, itakaa kufanya majumuisho yote.
Akizungumzia ushindi wake, Mdee alisema wanawake wengi wamekuwa waoga kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na ushindi wake huo, ni chachu kwa wasichana wengine kuona kuwa wanaweza na fursa zipo wazi.
“Chaguzi bado zinaendelea na mpaka sasa bado hatujapata timu kamili, hivyo timu ikikamilika tutaweka wazi mikakati mbalimbali ya kumuinua mwanamke,” alisema.

Alisema watafanya ziara ya miezi miwili nchi nzima kuzungumza na wanawake ili wajitambue na kutambua kuwa Chadema ndio chama pekee kitakacholeta maendeleo.

No comments:

Post a Comment