Rais wa Liberia Sirleaf Johnson amewafuta kazi
maofisa kumi wa serikali kwa kukataa kurudi nchini humo wakati ambapo
taifa hilo linakabiliana na maambukizi hatari ya ugonjwa wa Ebola.
Maafisa hao waliagizwa kurudi nchini humo mwezi mmoja uliopita.Rais Sirleaf amewashutumu kwa kutojali janga
linalowakumba raia wa taifa hilo.
Bi Sirleaf ameripotiwa kuomba msaada zaidi kwa serikali ya Rais Obama ili kukabiliana na virusi hivyo.
Ameitaka Marekani kujenga kituo kimoja cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.
Virusi hivyo vimewaua zaidi ya watu 2,400 Magharibi mwa Afrika tangu mwezi Machi ,nusu ya raia hao wakitoka nchini Liberia.
BBC/SWAHILI

No comments:
Post a Comment