CUF:TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
11/09/2014
Kifungu
21 cha Azimio la Haki za Binaadamu duniani kinatamka kwamba “Matakwa na
utashi wa watu utakuwa ndio msingi wa mamlaka ya Serikali, matakwa haya
yatathibitishwa na uchaguzi ndani ya vipindi mbali mbali. Uchaguzi huo
utakuwa sawa kwa wote na kutoa haki ya kuchagua na utafanywa kwa kura ya
siri au kwa utaratibu mwengine ulio huru“
Kifungu hiki kinaweka kanuni ya msingi ya usawa wa kuchagua (kupiga kura) au kupata uwiano wa uwakilishi na ndio msingi mmoja kati ya misingi ya kuwepo kwa mipaka ya majimbo ya uchaguzi duniani kote.
Kifungu hiki kinaweka kanuni ya msingi ya usawa wa kuchagua (kupiga kura) au kupata uwiano wa uwakilishi na ndio msingi mmoja kati ya misingi ya kuwepo kwa mipaka ya majimbo ya uchaguzi duniani kote.
Mamlaka ya Tume
Tume
ya uchaguzi Zanzibar ndio chombo kilicho na mamlaka ya kusimamia
chaguzi zote za Wananchi na kura ya maoni zinazofanywa Zanzibar. Kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, toleo la mwaka 2010 Tume
imepewa mamlaka na vigezo vya kuzingatia katika kuongeza au kupunguza
majimbo ya uchaguzi kwa kutilia maanani sababu mbali mbali. Kifungu cha
120 cha Katiba hiyo kinasema:-
1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu hiki, Zanzibar inaweza kugaiwa katika majimbo ya uchaguzi yenye majina na mipaka kama yatakavyoelezwa na Tume.
1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu hiki, Zanzibar inaweza kugaiwa katika majimbo ya uchaguzi yenye majina na mipaka kama yatakavyoelezwa na Tume.
2)
Baraza la Wawakilishi linaweza kuweka kisheria, idadi ndogo kabisa ya
majimbo ya uchaguzi yasiyopungua 40 na idadi kubwa kabisa ya majimbo
yasiyozidi 55.
3)
Majimbo yote yatakuwa karibuni na wakaazi sawa sawa kama
itakavyoonekana na Tume, lakini Tume inaweza kuepuka shuruti hii kwa
kiwango kile kinachofikiria kuwa inafaa kwa ajili ya kuzingatia:
a) idadi ya watu na zaidi katika kuhakikisha uwakilishi unaofaa katika miji mikubwa na miji ya mashamba yenye idadi ndogo ya watu;
b) ukuaji wa idadi ya watu;
c) njia za usafiri;
d) mipaka ya sehemu ya utawala, na kwa madhumuni ya kifungu hiki idadi ya wakaazi wa sehemu yoyote ya Zanzibar itahakikishwa na ripoti ya kuhesabu watu ya karibuni sana ambayo imefanywa kwa mujibu wa sheria.
4)
Katika kipindi cha miaka 8 hadi 10 au wakati wowote Tume itachunguza
idadi ya mipaka na majina ya majimbo hayo kwa kiwango kile ambacho
inahisi ni wajibu kuangaliwa upya, na inaweza kwa kutoa tangazo,
kubadili idadi, mipaka na majina ya majimbo hayo.
5) Iwapo hesabu ya idadi ya watu imeshafanywa kwa mujibu wa sheria, au iwapo mabadiliko yamefanywa katika mipaka ya sehemu yoyote ya Utawala, Tume inaweza ikachunguza suala hilo na kuweka mabadiliko hayo katika kiwango kile ambacho Tume inahisi ingefaa kufanyiwa mabadiliko hayo.
Kwa
kutumia Mamlaka iliyotajwa hapo juu, Tume ya Uchaguzi Zanzibar imepitia
na kuyagawa upya Majimbo ya Uchaguzi Zanzibar katika vipindi tofauti
vya muda. Kwa Mfano Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka 2000 Majimbo
ya Malindi, Mkunazini na Makadara yaliyokuwemo katika orodha ya Majimbo
ya Wilaya ya Mjini yalifutwa na badala yake Tume ikaanzisha Majimbo
Mapya ya Mji Mkongwe, Chumbuni na Dole.
Kwa
kutumia kigezo cha Sensa ya mwaka 2002, ambapo Zanzibar ilikuwa na
idadi ya watu 981,754, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilifanya upitiaji
upya wa majimbo ya uchaguzi mwaka 2005, ambapo katika zoezi hilo baadhi
ya majimbo yalibadilishwa majina na mipaka mipya kuongezwa. Majimbo ya
Mwera, Muembemakumbi, Mlandege, Utaani, Vitongoji, Wingwi na Pandani
yalifutwa, na Majimbo mapya ya Magogoni, Bububu, Fuoni, Kiembesamaki,
Mtoni, Mwanakwerekwe, Mpendae na Wete yakaanzishwa.
Wakati
Tume ikifanya zoezi hili ilizingatia kigezo cha idadi ya watu pekee na
kuacha kuzingatia vigezo vingine vya kikatiba kama inavyotakiwa na
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Aidha,
kigezo hiki cha idadi ya watu kinaonekana kutumiwa kwa utashi wa
kisiasa kwani wakati wa zoezi hilo kilitumika katika kuyagawa majimbo ya
baadhi ya wilaya mfano majimbo ya wilaya ya Wete, na kuacha kutumiwa
katika wilaya nyengine kama vile majimbo ya wilaya ya Kaskazini ‘A’
Upitiaji huo wa Majimbo ya uchaguzi Zanzibar ulioshindwa kuzingatia vigezo vya kikatiba ulisababisha
i. Kuwepo kwa uwakilishi usio sawa. Hii ilitokea pale wakati wa upunguzaji wa majimbo zaidi kwani kura za waliokuwa wakishinda huenda zikapotea baada ya jimbo lao kuondolewa na tume. Mfano ubadilishaji wa mipaka ya Jimbo la Kikwajuni mwaka 2000 kwa kuliongezea baadhi ya shehia nje ya jimbo hilo (shehia ya Miembeni) kwa ajili ya kukisaidia Chama Tawala ulipelekea kutokea kwa tatizo hilo.
i. Kuwepo kwa uwakilishi usio sawa. Hii ilitokea pale wakati wa upunguzaji wa majimbo zaidi kwani kura za waliokuwa wakishinda huenda zikapotea baada ya jimbo lao kuondolewa na tume. Mfano ubadilishaji wa mipaka ya Jimbo la Kikwajuni mwaka 2000 kwa kuliongezea baadhi ya shehia nje ya jimbo hilo (shehia ya Miembeni) kwa ajili ya kukisaidia Chama Tawala ulipelekea kutokea kwa tatizo hilo.
ii. Sauti za kura au maamuzi ya wapiga kura kutokuwa na thamani. Mara nyingi kura huwa ni kielelezo cha maamuzi ya watu kupata kiongozi wao au kufanya maamuzi katika maendeleo ya jamii yao. Ugawaji na ukataji wa majimbo uliofanywa na Tume ya uchaguzi kwa miaka iliyopita uliegemea mrengo wa kisiasa na hivyo kufanya kura za watu fulani au kundi fulani zisionekane athari yake katika maamuzi husika.
iii.
Kuondoka kwa ushawishi na mchango wa chama ambacho mawazo yake
hayazingatiwi katika maamuzi ya uendeshaji wa chaguzi. Kila kundi ndani
ya jamii lina nafasi yake katika kukuza demokrasia na Maendeleo ya siasa
na uchumi. Mfumo usio makini uliotumika katika mchakato wa kuongeza au
kupunguza ama kubadili mipaka ya majimbo kwa lengo la kusaidia kundi
fulani, umepelekea kudumaa kwa siasa za ushindani na hivyo kudumaza
maendeleo na ustawi wa watu katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.
SABABU ZA KUKUTANA NA WANAHABARI
1.CUF-Chama
Cha Wananchi kinatambua mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa
habari katika shughuli za maendeleo, vyombo vya habari katika ulimwengu
wetu wa leo vimekuwa ni kiunganishi kikubwa kati ya jamii na taasisi
mbali mbali.
2. Katika siku za hivi karibuni, Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar amesikika akisema kwamba ni Wananchi tu ndio ambao wametoa maoni juu ya zoezi la upitiaji na ugawaji wa majimbo. CUF imeamua kukutana na wanahabari kuwaeleza kwa uwazi kwamba iliwasilisha nyaraka mbili ambazo zinajitosheleza kimaelezo juu ya upitiaji, ugawwaji na ubadilishaji wa majimbo na wadi za uchaguzi kwa namna ambayo kwa namna ambayo itasaidia ugawaji bora wa majimbo ya uchaguzi Zanzibar.
3.CUF-Chama Cha Wananchi kimelazimika kukutana na wananhabari kuelezea wasi wasi wake juu ya taarifa za Tume ya Uchaguzi Zanzibar kujenga mazingira ya kuhalalisha kutumia maoni ya chama tawala katika ugawaji na upitiaji wa majimbo kinyume na utaratibu wa sheria na hivyo kuwa mwanzo wa uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 2015.
UDHAIFU WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR KATIKA MAPITIO NA UGAWAJI WA MAJIMBO MIAKA ILIYOPITA
Katika ugawaji wa mipaka ya majimbo ya uchaguzi uliofanywa na Tume mwaka 2000 na 2005 kasoro zifuatazo zilijitokeza:
i.Kuzingatiwa kwa kigezo kimoja cha idadi ya watu na kutotilia maanani vigezo vingine vya kikatiba. Mfano kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010 Tume ya uchaguzi imetakiwa, pamoja na mambo mengine, kuhakikisha uwakilishi unaofaa katika miji mikubwa na miji ya mashamba yenye idadi ndogo ya watu.
i.Kuzingatiwa kwa kigezo kimoja cha idadi ya watu na kutotilia maanani vigezo vingine vya kikatiba. Mfano kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010 Tume ya uchaguzi imetakiwa, pamoja na mambo mengine, kuhakikisha uwakilishi unaofaa katika miji mikubwa na miji ya mashamba yenye idadi ndogo ya watu.
Ugawaji
wa majimbo mwaka 2005 kwa kiasi kikubwa ulishindwa kuzingatia kigezo
hicho. Majimbo ya wilaya za Wete, Chake chake, na Micheweni yaliyofutwa
yalikuwa na sifa za miji ya mashamba.
ii.Kuzingatiwa
kwa baadhi ya vigezo kwa baadhi ya majimbo na kupuuzwa katika majimbo
mengine. Mfano, kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2002,
Mkoa wa kaskazini Unguja ulikuwa na idadi ya watu 136,639 na kupaswa
kuwa na majimbo saba, lakini Tume iliamua kuweka majimbo nane ya
uchaguzi katika wilaya hiyo.
Kwa
mujibu wa gazeti la Nipashe toleo namba 0578232 la Jumatano septemba
10, 2014, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salim Jecha, alisema kuwa yapo
baadhi ya majimbo yana idadi kubwa ya wakaazi na yanastahili kukatwa na
kuwa majimbo mawili tofauti na majimbo mengine yana idadi ndogo ya
wakaazi yanastahili kukatwa mfano majimbo mawili kufanywa jimbo moja.
Aidha,
Mkurugenzi wa tume hiyo, Salum Kassim Ali, alitaja majimbo kama vile
Dimani lenye idadi ya wananchi 58,000, Fuoni lenye Wananchi 65,000 na
Dole lenye wananchi 39, 000 kuwa ni majimbo yanayoongoza kwa na idadi
kubwa ya watu na majimbo ya Mgogoni lenye idadi ya watu 17,000, Chambani
lenye idadi ya watu 15, 000 na Raha Leo lenye idadi ya watu 16,000 kuwa
ni majimbo yenye idadi ndogo ya watu.
Taarifa
za Tume ya uchaguzi Zanzibar juu ya idadi ya watu katika majimbo ya
uchaguzi, kama zilivyochapishwa na vyombo vya habari, ni za upotoshaji
na zinazokwenda kinyume na taarifa mbalimbali za serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012, jimbo
la Mgogoni lina idadi ya watu 21, 649 badala 17,000, Chambani kuna
wakaazi 15, 909 badala ya 15, 000 na Dole lina watu 38, 775 badala ya
39, 000 kinyume na madai ya Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar.
Mbali
ya kupewa mamlaka ya kutumia vigezo mbalimbali kwa mujibu wa katiba ya
Zanzibar, Tume imekuwa ikitumia zaidi kigezo cha idadi ya watu katika
kuyagawa majimbo ya uchaguzi Zanzibar. Kigezo hiki hakitokuwa na mantiki
ya kutumika kwa sasa. Kwa mujibu wa Takwimu za sensa ya watu na makaazi
ya mwaka 2012 hakuna ushahidi wa kupungua kwa idadi ya watu katika
wilaya na mkoa wowote wa Zanzibar, bali ongezeko kubwa la idadi ya watu
katika maeneo hayo.
Aidha,
sensa ya mwaka 2012 ilifanyika baada ya miaka kumi (2002-2012) kinyume
na sensa ya mwaka 2002 ambayo ilifanyika baada ya miaka 14 (1988-2002),
hivyo kulinganisha ongezeko la idadi ya watu na kugawa majimbo kwa
kigezo cha idadi ya watu kwa kutumia sensa hizi mbili hakutakuwa na
mantiki ya msingi.
Kuwepo
kwa idadi ya majimbo yenye watu wengi na hivyo kukosekana uwiano
sawasawa wa uwakilishi wa wananchi katika majimbo ya uchaguzi kutoka
jimbo moja hadi jingine, kama inavyoelekezwa na katiba, kunatokana na
mfumo mbaya ulioshindwa kuzingatia vigezo vya kikatiba na kimazingira
katika kuyagawa majimbo ya uchaguzi katika miaka iliyopita kwa lengo la
kukihakikishia chama tawala ushindi.
Aidha
maelezo ya Tume ya uchaguzi yanathibitisha uwepo wa lengo la kugawa
majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu na kupuuza
vigezo vyengine vya msingi vya kikatiba kama vile uwiano wa uwakilishi
wa miji mikubwa na miji ya mashamba yenye idadi ndogo ya watu, njia za
usafiri na mipaka ya sehemu ya utawala kama ilivyojitokeza katika
ugawaji wa majimbo ya uchaguzi katika miaka iliyopita.
Kama
ilivyoainishwa, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imepewa mamlaka ndani ya
katiba kuhakikisha uwakilishi unaofaa katika miji mikubwa na miji ya
mashamba yenye idadi ndogo ya watu. Hichi ni kigezo kimojawapo ambacho
Tume inaweza kukizingatia kwa kutengua shuruti ya uwakilishi sawa sawa
wa idadi ya watu katika kuyagawa majimbo na mipaka yake. Majimbo
yanayoelezwa na Tume ya uchaguzi kuwa na idadi ndogo ya watu, kama
ilivyochapishwa na vyombo vya habari, yana kidhi haja na sifa ya kubaki
kama yalivyo kutokana na kuwa na sifa ya kuwa ni majimbo ya mashamba
kama inavyotakiwa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, toleo la 2010.
Kufutwa
kwa majimbo yanayodaiwa kuwa na idadi ndogo ya watu kwa kuchanganywa na
kuwa jimbo moja, kutapelekea kupunguza uwiano wa uwakilishi wa Wananchi
katika vyombo vya uwakilishi na maamuzi. Uzoefu unaonesha wazi kwamba
Tume ya Uchaguzi mara zote imekua ikiegemea hoja ya idadi ya watu na
kusahau hoja nyengine zilizomo ndani ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa
katiba.
Upitiaji
wa mipaka ya Majimbo uliofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar mwaka 2005
na kupelekea kufutwa kwa majimbo ya Mwera, Utaani, Vitongoji, Wingwi na
Pandani kwa kigezo cha idadi ya watu bila ya kuzingatia kwamba ni
majimbo ya miji ya shamba yenye tofauti kubwa na miji mikubwa.
Aidha,
maelezo ya Tume yanadhihirisha muendelezo wa mpango wa ukiukwaji wa
sheria na utendaji wa upendeleo kama inavyothibitishwa na matokeo
mbalimbali ya uvizaji wa demokrasia nchini. Mfano wa karibu wa
kuthibitisha jambo hili ni matukio yaliyojitokeza baada ya zoezi la
uandikishaji na uwekaji wazi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Baada
ya kumalizika kwa mara ya pili kwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura,
Tume kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 1984,
kifungu cha 25 (i), ilitangaza ruhusa ya pingamizi kwa walioandikishwa
bila ya kukidhi sifa na vigezo vya haki ya kuandikishwa.
Mfano
wa mipango ya uchafuzi wa uchaguzi mkuu wa 2015 unadhihirika katika
jimbo la Tumbatu ambapo katika malalamiko ya pingamizi 288
yaliyoripotiwa katika Tume ya uchaguzi katika jimbo hilo, ni watu 12 tu
ndio waliyoondoshwa katika daftari kama inavyoonekana katika jadweli
lifuatalo:
Nam Shehia Pingamizi zilizowekwa Pingamizi zilizosikilizwa Pingamizi zisizosikilizwa Waliofutwa katika daftari waliobaki
Nam Shehia Pingamizi zilizowekwa Pingamizi zilizosikilizwa Pingamizi zisizosikilizwa Waliofutwa katika daftari waliobaki
1. Pale 225 91 134 2 223
2. Mto wa pwani 63 19 44 10 53
JUMLA 288 110 178 12 276
Kutokana
na kasoro hizo na dalilili mbalimbali zilizojitokeza kama ilivyoelezwa,
The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinaitaka Tume ya
uchaguzi kuzingatia matakwa ya kikatiba na kuweka kwa uwazi uwiano wa
kimajimbo ili kuhakikisha uwakilishi bora wa wananchi katika vyombo vya
maamuzi na kutunga sheria kwa kuweka asilimia ambayo jimbo linaweza
kutofautiana na jimbo jengine (percentage of deviation) kwa idadi ya
watu.
Aidha,
CUF inaitaka Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kuzingatia kuwa kumekuwepo na
malalamiko ya muda mrefu ya wadau wa uchaguzi juu ya utaratibu mbovu wa
ugawaji wa majimbo Zanzibar kulikopelekea uvunjifu wa amani
kulikotokana na kutokuridhika kwa baadhi ya wananchi.
Ili
kuiepusha nchi na watu wake kurudi katika zama za khasama, chuki na
mifarakno, CUF-Chama Cha Wananchi kinaishauri Tume kuzingatia matakwa ya
Katiba na kufanya kazi zake kwa uadilifu na kutopokea maagizo yoyote
nje ya mamlaka yake katika kusimamia zoezi la uongezaji au upunguzaji au
ubadilishaji wa mipaka ya majimbo ya uchaguzi ili kuimarisha ustawi wa
demokrasia ndani ya Zanzibar.
Kutokana
na maelezo yaliyoainishwa hapo juu, The Civic United Front (CUF-Chama
Cha Wananchi) kinaitaka Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kuzingatia
mazingira ya amani na maelewano yaliyopo na kutokuwa taasisi ambayo
itakuwa chanzo cha vurugu na mifarakano katika nchi.
IMETOLEWA NA:
MH. NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU CUF- ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment