Ben Saanane
Henry Kilewo
Uamuzi huo unaonekana kuwashangaza wengi kutokana
na ukweli kwamba makada hao ndio kwa muda mrefu wamekuwa mstari wa mbele katika harakati mbalimbali ndani ya chama hicho, huku wengine wakihusishwa na migogoro iliyotokea huko nyuma.
Ben Saanane, ambaye inaelezwa kwamba amejipatia umaarufu mkubwa kupitia mgongo wa Zitto Kabwe akitajwa kama kijana wake wa karibu licha ya kukanusha mara kadhaa, anastahili kujipanga upya kuwania uongozi kwani mwaka 2009 alishindwa katika nafasi ya Uenyekiti wa Bavicha.
Hali hiyo ilitokana na tetesi kwamba alikuwa mtu wa karibu na Zitto Kabwe, ambaye wakati huo alikuwa ametangaza kugombea nafasi ya uenyekiti wa taifa kabla ya kushauriwa na wazee wa Chadema kuondoa jina lake.
Lakini pamoja na kuwa karibu na viongozi wakuu wa chama hicho tangu kufukuzwa kwa Zitto Kabwe, bado Saanane ameshindwa kupitishwa kugombea uongozi wa Bavicha baada ya jina lake kuondolewa kwa mizengwe, na sasa ameondolewa pia hata kuwania ujumbe wa kamati kuu kwa maelezo kwamba hana sifa.
Kwa upande wa Kilewo, ambaye anakumbukwa kwa kuhusishwa na tukio la kigaidi la kummwagia tindikali kijana mmoja huko Igunga kabla ya kushinda kesi, naye ameenguliwa kuwania ujumbe wa kamati kuu. Anakumbukwa pia kwa kubuni mradi uliopigwa marufuku na serikali wa TelexFree.


No comments:
Post a Comment