Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 15 September 2014

AICC YAKARIBISHA WAWEKEZAJI


Na Grace Macha, Arusha


KITUO cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), kimesema kinamiliki maeneo makubwa ya ardhi hivyo kutoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kuyatumia kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo vyuo vikuu, majengo makubwa ya biashara na hoteli.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kituo hicho, Elishilia Kaaya, wakati wa uzinduzi wa majengo mawili
ya ghorofa kwa ajili ya makazi ya kisasa yenye uwezo wa kutumiwa na familia 48, ambayo yamegharimu Sh bilioni 5.21.
Alisema kuwa, uwekezaji unaofanywa na kituo hicho, mbali ya kunufaisha wakazi wa jiji hapa lakini pia unaifanya Arusha kuendelea kuwa kivutio kikubwa hasa ikizingatiwa kuwa mashirika mengi ya kimataifa yanaendesha shughuli zao, hivyo wanaitumia fursa hiyo adhimu kuvutia mashirika mengi zaidi.
“AICC ni shirika lenye ardhi kubwa mkoani Arusha, hivyo napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali waje wawekeze katika maeneo ambayo yameainishwa katika ‘AICC Investment Prospectus’ hasa miundombinu ya kimaendeleo kama vile vyuo vikuu, majengo makubwa ya kibiashara, hoteli,” alisema Kaaya.
Alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyo maeneo ya Fire na Corridor, umefanyika ndani ya miaka miwili ambako kwenye fedha zilizotumika kugharamia ujenzi huo Sh bilioni 1.960 ni fedha zinazotokana na mapato yao ya ndani huku Sh bilioni 3.250 ni mkopo kutoka benki ya NBC.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika hafla hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa ya Arusha, Jowika Kasunga, aliwataka wadau mbalimbali yakiwemo mashirika  nchini, kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa nyumba ili kuwezesha kuondoka na changamoto ya ukosefu wa nyumba uliopo nchini.
CREDIT: TANZANIADAIMA

No comments:

Post a Comment