Upasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani.
Upasuaji
huo wa saa 12- utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa ya damu
kwa ajili ya kutunza mkojo na kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo la
ngono.Upasuaji huu unafuatia mafanikio ya kwanza kabisa ya upandikizaji wa uume nchini Afrika kusini mwaka jana.
Jopo la madaktari kutoka Hospitali ya chuo kikuu cha Hopkins (JHU) wanapanga kumfanyia upasuaji huyo mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 60kama sehemu ya majaribio.
Hatua ya kwanza ya upasuaji huo itaanza kwa kuondoa uume kutoka kwa kijana aliefariki ambaye alijitolea kutoa uume wake kwa ruhusa ya familia yake.
Kwa mujibu wa jopo la madakatari katika JHU matumaini ya mwanajeshi huyo wa zamani ni kwamba hisia za uume wake zitarejea katika muda wa miezi 12.
Uwezekano wa mgonjwa kupata watoto, utategemea kiwango cha jeraha na mafanikio ya upasuaji huo.
Lakini Wanasayansi wanasema kutokana na kwamba ni upasuaji mmoja wa kupandikiza uume uliofanyika, madaktari watakua makini kuhakikisha kuna matumaini ya kweli.
BBC
No comments:
Post a Comment