Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 12 December 2015

MTOTO WA KIM NA KANYE WEST ANAITWA SAINT WEST!

Mtoto wao wa kwanza anaitwa North West 
 
Kim Kardashian West na Kanye West wamempa mtoto wao wa pili jina Saint West.
Kim amethibitisha jina hilo kwenye tovuti yake, siku tatu baada ya kutangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume.

Binti wao, aliyepewa jina North West, alizaliwa Juni 2013.
Kim alitangaza kwamba alikuwa ameshika mimba mara ya pili kwenye kipindi chake cha runingani cha Keeping Up with the Kardashians mwishoni mwa mwezi Mei.
Alifichua kwamba mtoto wake wa pili angekuwa mvulana kwenye ujumbe aliomuandikia Kanye West kwenye Twitter siku ya kuwakumbuka kina baba duniani, yaani Father's Day.
Wawili hao hawajasema ni kwa nini wakachagua jina Saint West lakini baadhi ya ripoti zinasema ni kwa sababu Kim alisumbuka sana alipokuwa na mimba yake.
Kim Kardashian alisumbuliwa sana na mimba ya mtoto wake wa pili
Jina la mtoto huyo limevuma sana kwenye Twitter muda mfupi baada ya kutangazwa, baadhi wakilifurahia.

BBC

No comments:

Post a Comment