Na Ezekiel
Kamanga, Mbeya
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imememhukumu kwenda jela miaka mitatu Martin Mhina
Dereva wa basi la Majinja kwa kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali iliyoua mtu mmoja.
Waendesha
Mashitaka wa Serikali Hannarose Kasambala na Catherine Gwatu wameiambia
Mahakama kuwa Dereva huyo aliendesha Basi la Kampuni ya Majinja kwa uzembe
mapema mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi kwa kuigonga gari aina ya Toyota
Hilux na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Mawakili hao
wameiambia Mahakama kuwa Kesi hiyo namba 46/2015 ambapo Dereva huyo alitenda kosa
hilo kinyume cha Sheria ya usalama barabarani namba
40(1),63(2)(a),27(1)(a)III(c) kifungu cha 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Akijitetea
mbele ya Mahakama Martin ameiomba Mahakama kumsamehe kwa kuwa hilo ni kosa lake
la kwanza na kwamba anayo familia inayo mtegemea hivyo imwonee huruma kutokana
na kosa hilo.
Baada ya
kupitia ushahidi uliotolewa Mahakamani na Upande wa Mashitaka na utetezi wa
Mshitakiwa Hakimu Zawadi Laizer alimtia hatiani kutumikia kifungo cha miaka
mitatu jela ili iwe fundisho kwa madereva wasifuata sheria za usalama
barabarani.
No comments:
Post a Comment