Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 22 March 2015

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI BABATI MKOANI MANYARA


1a
Mkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati, kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
2a
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
3a
Baadhi ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.
5a
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
6a
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
7a
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.
8a
Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.

No comments:

Post a Comment