Mmoja wa msikiti katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Balozi wa Marekani katika umoja wa
mataifa anasema kuwa karibia misikiti yote katika jamhuri ya Afrika ya
kati imeharibiwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliovyoanza
miaka miwili iliopita.
Samantha Power ambaye alilitembelea taifa hilo wiki iliopita amesema kuwa ni misikiti 19 pekee kati ya 436 iliosalia.
Vita vingi vimekuwa kati ya waislamu na wakristo.
Bi Power ameonyesha wasiwasi kuhusu ukosefu wa usalama huku vikosi vya Ufaransa na vile vya muungano wa Ulaya vikiondoka nchini humo kabla ya kikosi kamili cha Umoja wa mataifa kupelekwa.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment