Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 16 March 2015
"CCM, WATENDAJI WAGEUKA KERO KWA WAFUGAJI"
Na Hastin Liumba,KaliuaMBUNGE wa viti maalumu kupitia chama cha wananchi (CUF) Magdalena Sakaya amesema baadhi ya watendaji na CCM ni kero kubwa kwa wananchi jamii ya wafugaji wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Akiongea na wananchi wa wilaya ya Kaliua kwenye mkutano wa hadhara Sakaya alisema maeneo yote aliyopita amekuta kero kubwa ya wafugaji wakilalamikia watendaji wa serikali na wale wa CCM kuwachangisha fedha mara kwa mara.
Sakaya alifafanua watendaji baadhi wa serikali wamekuwa wakiwachagisha fedha ambazo mara kadhaa hawapewi risiti na wale wa CCM wanawachangisha fedha wakiwaeleza watawasadia waendelee kuwepo kwenye maeneo wanaoishi wakidaiwa wapo ndani ya hifadhi.
Mbunge huyo wa viti maalumu (CUF) alifafanua na kuwataka wananchi hao kubadilika bila kufanya makosa kwani safari hii ameamua kuchukua fomu kugombea ubunge wa jimbo la Kaliua ambalo kwa sasa lipo chini ya Profesa Juma Kapuya.
“Ndugu zangu safari hii msifanye makosa mkachagua CCM……kero mliyonayo hamtaiondosha na mtaendelea kumia na kulalamika tu fanyeni mabadiliko sasa msidanywe na viongozi wa CCM kwa kuwapa kadi halafu mnakuja kujuta.”alisema Sakaya.
Alisema amefanya ziara mara kadhaa kero kubwa kwa sasa ni sekta ya afya na wafugaji na zaidi wafugaji wanateswa wanapigwa risasi wanachangsihwa risiti hawapewi haya yote yanafanyika hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika.
Sakaya alisema kote alikopita na kukutana na jamii ya wafugaji wamemweleza watafikia mahali watahamia nchi jirani wanayoona itawafaa maana Tanzania wanaona si salama kwao.
Alisema wamemweleza kwa uchungu na masikitiko makubwa kuona ndani ya ardhi yao wanaishi kama wakimbizi hivo suluhu kwao ni kuhama Tanzania.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kaliua Kasele alipoulizwa juu ya chama chake kushutumiwa kugeuza wafugaji kitegauchumi alikana tuhuma hizo na kusema ni siasa za maji taka.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Venance Mwamoto alipotaftwa hakupatikana kwani ilidaiwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment