Timu
ya Taifa ya soka la Ufukweni (Beach Soccer) imewasili salama jijini Cairo
nchini Misri tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa
fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli.
Msafara
wa timu ya soka la Ufukweni ulipokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania
waliopo nchini Misri, pamoja na viongozi
wa chama cha soka nchini Misri (EFA).
Leo
jioni kikosi kinatarajia kufanya mazoezi mepesi, kabla ya kesho kufanya mazoezi
ya mwisho katika uwanja utakaofanyika mchezo siku ya jumapili.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF linaitakia kila la kheri timu ya soka la ufukweni
katika mchezo wake wa marudiano siku ya jumapili dhidi ya Misri.
No comments:
Post a Comment