Mkuu
wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akiangalia namna pombe ya kienyeji
inavyoandaliwa baada ya kukamata kiwanda bubu cha kutengenezea pombe
bila ya kufuata taratibu.
Mmiliki
wa kiwanda cha kutengeneza pombe ya kienyeji aliyefahamik kwa jina
moja la Carlos akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo
namna wanavyoandaa pombe hiyo.
Carlos
akifungua madumu makubwa yaliyohifadhi Pombe ya Kienyeji wakati wa
utengenezaji wake katika kijiji cha Useri wilayani Rombo.
Kreti za Chupa za Banana ambazo zimekuwa zikitumika pia katika kuwekea pombe hiyo mara baada ya kutengenezwa.
Askari Mgambo akiweka ndizi zilizovundikwa katika ndoo ambazo pia hutumika katika utengenezaji wa pombe hiyo ya kienyeji.
Nyumba
ambayo imekuwa iktumika kutengenezea Pombeza kienyeji kulipokutwa
mitambo wa kutegeneza pamoja na pombe iliyokuwa katika maandalizi.
Mkuu
wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akimwaga pombe ya kienyeji iliyokuwa
ikiandaliwa katika moja ya kiwanda bubu kilichokutwa katika kijiji cha
Useri wilayani humo.
Katibu
tawala wa wilaya ya Rombo ,Abubakar Asenga akimwaga pombe hiyo mara
baada ya kufanya operesheni ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali ya
wilaya ya Rombo.
Katibu
tawala wa wilaya ya Rombo,Abubakar Asenga akipakia madumu makubwa
yaliyokutwa yakitumika katika utengenezaji wa Pombe katika kijiji cha
Useri wilaya Rombo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment