Halmashauri ya jiji la Arusha imeokoa zaidi ya shilingi milioni mia tatu
sitini na nne zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuwapa wakandarasi kwa ajili ya kujenga madarasa baada yake kamati za shule kupewa jukumu la kusimamia ujenzi wa madarasa hayo badala ya mkandarasi.
Hayo yamebainishwa na meya wa halmashaur i ya jiji la Arusha Kalist Lazaro wakati akiongea na waandish I wa habari ambapo alisema kuwa halmashauri yake wamekaa chini na kuona kuliko fedha hizo zipewe wakandasi ili wajengee madarasa ni bora fedha za ujenzi wa madarasa zipelekwe katika kamati za shule pamoja na bodi za shule ili wasimamie ujenzi huo.
Alisema kuwa sasa ivi halmashauri imetoa shilingi bilioni moja laki nne kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ya shule za msingi na fedha zote zilishapelekwa katika kamati za shule ili waweze kusimamia ujenzi mpaka ukamilike.
“Zamani tulikuwa tunatumia wakandarasi kwa kutangaza tenda kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule za msingi ,lakini tangu tuanze kujenga madarasa kwa kupitia kamati za shule na sio wakandarasi tumekuwa tunaokoa milioni mia tatu sitini nne ambazo tumeziokoa tungetumia wakandarasi zote zingeingia katika mfuko wa mkandasi sasa ndio maana tumeamua kumtumia kamati za shule kwa shule za msingii “alisema Kalist
Aidha alisema kuwa jiji la Arusha kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto ambao wanaandikishwa darasa la kwanza tuofauti na mwaka huliopita kwani tangu zoenzi limeanza adi kufikia sasa wameshaandikisha wanafunzi wa darasa la kwaza zaidi ya elfu 12000 tofauti na mwaka uliopita 2016 ambapo watoto elfu tisa mia sita na mia waliandikishwa kuingia darasa la kwanza , ambapo alisema bado wanaendelea kuandikisha watoto adi mwezi march ili watoto wote waweze kwenda shule
Alisema kuwa kutokana na kuwepo na watoto wengi waliojiandikisha kumekuwa na upungufu wa madarasa hivyo halmashauri imejenga madarasa 56 kwa ajili ya watoto hao wapya na kukarabati madarasa manne ya shule ya msingi ambayo yatasaidia kabisa kumaliza tatizo hili,ambapo alisema kuwa pia madarasa hayo yanaitaji madawati na hadi sasa halmashauri imeshatoa fedha kwa ajili ya madawati 1380 ambayo watoto hao watakalia katika madarasa hayo mapya hivyo wanaimani kuwa watoto wote wanaoanza darasa la kwanza wataingia madarasani na kukaa katika madawati na kusoma vizuri kama vile inavyotakiwa.
Akifafanua kuhusu wanafunzi wa shule za sekondari alisema kuwa jiji la Arusha lilifaulisha kwa asilimia 92% wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na kukakuwepo na upun gufu wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi hao lakini jiji limeshajipanga vyema na imeanza kujenga madarasa 25 kwa ajili ya shule za sekondari na kiasi cha shilingi milioni 700 zimeshatumwa katika bodi za shule hizo na wanaimani adi ifike mwisho wa mwezi huu wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza wataingia madarasani na kuendelea namasomo kama kawaida.
“Napenda ku sema kuwa hakuna mtoto ambaye amefaulu kuingia kidato cha kwanza ataacha kuingia darasani ifikapo mwisho wa mwezi huu madarasa yatakuwa tayari na wanafunzi wote waliofaulu wataenda shule “alisema Kalist.
No comments:
Post a Comment