Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa
(UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo wakati viongozi wa Mahakama hiyo walipomtembelea
kiongozi huyo wa Wizara, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo.
Katikati ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT),
Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili kushoto) na Msajili wa Mahakama hiyo,
Dk. Elias Olufemi (kushoto), wakati walipomtembelea Wizarani kwa lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa
(UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (kulia) wakati alipokuwa akifafanua
jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara
hiyo. Wapili kulia ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi. Mazungumzo
hayo yalifanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam leo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (watatu kulia), Mkuu wa
Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili
kulia), Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi (watatu kushoto), wakiwa
katika picha ya pamoja na maafisa wengine mara baada ya Mhandisi Masauni
kufanya mazungumzo na ujumbe huo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
*****************************************************************************
No comments:
Post a Comment