MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye mazoezi hayo kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kujenga afya.
MKUU wa wilaya ya Muheza
Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki mazoezi ya
kuruka ikiwa ni kuunga mkono agizo la
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
leo kwenye uwanja wa
Jitegemee wilayani Muheza
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew mara baada ya kumalizika mazoezi hayo. |
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Jogging hiyo. |
MKUU wa Wilaya ya Muheza
Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatenga
maeneo ya viwanja vya
michezo ili kuwezesha vijana kushiriki kwenye michezo jambo
ambalo linaweza kuwasaidia
kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha.
Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya
mazoezi kila Juma mosi ya pili
ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili ya watumishi na vijana ili kuepukana
na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo
yanaweza kuwanyemelea.
Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo
kunapunguza fursa kwa wananchi
na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hata kuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu
ya kujipatia ajira.
“Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa
vijana wengi ambao asilimia
kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wa maisha”Aliseam Hajat Tumbo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga
alisema kuwa kumekuwepo na
ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu
wa kufanya mazoezi hasa kwa
watumishi wa Serikali.
“Laima tubadilike kwa kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa hayo ambayo yamekuwa pigo kwa wananchi na hasa watumishi wa Umma,inatulazimu tupambane kukabiliana na hali hiyo kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zetu”Alisema Dk Mathew.
Naye Katibu Tawala Wilaya hiyo Desderia Haule ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilya alisema zoezi hili litakuwa ni endelevu na Serikali itatenga maeneo ya kutosha ya viwanja kwa ajili mazoezi na kukuza vipaji vya vijana . Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment