Mlezi
wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini A, Unguja wakati wa Kufungua
Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake
wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo
Wana CCM wa Kaskazini A wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya
Uongozi yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Kaskazini A Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya
kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi yaliofanyika Mkokotoni Unguja
kwenye Chuo cha Amali.
...................................................................
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa
Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na
kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduz i(CCM) Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli
hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na watendaji wa CCM na Jumuiya
zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi, wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa
Kaskazini (A) Unguja.
Samia Suluhu
Hassan amesema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu
chama kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia CCM kusonga mbele
na kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.
Amesisitiza
wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na mikakati
imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na kushika dola.
Mjumbe huyo ambaye
pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini A Unguja amesema Umoja na
Mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio silaha madhubuti
itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na kuongeza maradufu idadi
ya wanachama nchini.
Amesema kwa
sasa Viongozi watakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha jumuiya za
chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri ili zianze
kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa pia ameendelea kuonya baadhi ya
viongozi waache tabia ya kutengeneza makundi ya ndani ya chama kwa ajili ya kusaka
madaraka bali wawe mstari wa mbele katika kujenga umoja na mshikamano ndani ya
chama.
Kuhusu
mafunzo, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wanaopata mafunzo hayo
kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi kwenye maeneo yao wanafanya kazi
kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa.
Amesema kwa
sababu Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ni
muhimu kwa viongozi wa chama katika ngazi zote washirikiane na viongozi wa Serikali
katika maeneo husika ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya wananchi inafanyika
kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha.
No comments:
Post a Comment