Baada ya mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa shindano la MISS KIBOSHO 2017 kufanyika kwa mara ya kwanza usiku wa ijumaa Januari 27, 2017 na jana jumamosi Januari 28,2017 katika Ukumbi wa Kibosho Luxury Bar Kiseke Ilemela Jijini Mwanza, hatimaye mshindi amejulikana.
Mshindi wa shindano hilo lililofana vyema alikuwa ni Kephlin Jacob (katikati), nafasi ya pili ni Aida Gazar (kulia) na nafasi ya tatu ni Careen Nestory (kushoto), ambapo wanyange hao walifanikiwa kupenya na kuibuka na ushini huo miongoni mwa wanyange 10 walioshiriki shinano hilo.
Miss Kibosho 2017 iliandaliwa na Raju Entertainment kwa ushirikiano wa karibu na Kibosho Luxury Bar and Guest House Kiseke, Wema Salon, Mama Ngenda Sakon, Top Model na Hangano Cultural Group lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji vya urembo kitaifa na kimataifa.
Na Binagi Media Group
Miss Kibosho 2017 Kephlin Jacob (katikati), Miss Kibosho 2017 nambari mbili, Aida Gazar (kulia) na Miss Kibosho nambari tatu ni Caren Nestory (kushoto).
Awali hatua ya tatu bora ilikwena kwa washiriki, Caren Nestory (kushoto), Kephlin Jacob (katikati) na Aida Gazar (kulia)
Awali washiriki waliotinga nafasi tabo bora ni Caren Nestory, Jackline Moses, Denzry Michael, Kelphine Jacob na Aida Gazar.
Washiriki wote 10 wa Miss Kibosho 2017 ambao ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.
No comments:
Post a Comment