Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisaini
daftari la wageni baada ya kuwasili wilayani Momba Mkoani Songwe, kwa lengo
la kutembelea na kukagua uingiaji na
utoakaji wa raia na wageni katika mpaka wa Tunduma unaotoa huduma kwa watu
wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini,
Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Afisa
Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na
kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC
Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu
wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana
pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara
za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika
ziara hiyo mkoani Songwe. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana
kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za
Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na
Polisi baada ya kutembelea mpaka wa Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa
pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment