Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km
50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame
Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na viongozi wengiene akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa
Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3)
kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe
la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa
Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili
Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani
Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Waziri wa TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa
barabara hiyo ya Mwigumbi-Maswa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Waziri wa TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Haji Omari Heri wakimwagilia maji mti mara baada ya kuupanda baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3),
mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiweka saini kwenye Ubao kwa kutumia Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki
cha Maswa Mkoani Simiyu. Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na
kuwashauri kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji
ya Chaki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia Wakazi wa Maganzo mkoani Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara
yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa mara baada ya kumaliza kuwahutubia
Wilayani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka wakiangalia utengenezwaji wa Chaki
katika kiwanda cha Chaki cha Maswa mkoani Simiyu. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment