Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Shaban Kaswaka (kushoto), akimtambulisha kwa wananchi Mgombea Udiwani kupitia chama hicho Kata ya Kijichi, Abdallah Shamas katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Temeke jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea Udiwani kupitia chama cha CUF wa Kata ya Kijichi, Abdallah Khalid Shamas akihutubia katika mkutano huo.
Wasanii wa kundi la Sanaa la Mwamuko wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
Wafuasi wa CUF wakimkaribisha mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi wakati alipokuwa amewasili kwenye mkutano wake wa kampeni.
Meza kuu katika mkutano huo.
wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Sera za CUF zikitolewa.
Mkutano ukiendelea.
Wafuasi wa chama cha CUF wakiinua mikono kukubali kumpigia kura mgombea wa chama hicho.
Na Dotto Mwaibale
MGOMBEA Udiwani Kata ya Kijichi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Khalid Shamas amewataka wananchi na wagombea wenzake kuacha siasa za chuki na chafu ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla.
Shamas alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Kijichi Dar es Salaam jana wakati akijinadi kwa wapiga kura.
"Siasa chafu za chuki na zinazowatenganisha wananchi kutokana na itikadi za vyama vyao hazifai na haziwezi kuleta maendeleo katika kata hiyo na taifa kwa ujumla" alisema Shamas.
Alisema siasa chafu zilizokuwepo katika eneo hilo la Mwanamtoti zilifikia hatua ya kugawana makaburi jambo ambalo lilikuwa ni hatari katika kushirikiana.
Akizungumzia baadhi ya vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo alisema cha kwanza ni kuhakikisha eneo la Mwanamtoti wanapata shule ya msingi ambayo itawasaidia watoto wa eneo hilo kutotembea umbali mrefu wa kwenda shuleni.
Alitaja kipaumbele chake cha pili ni kuhakikisha eneo hilo linapata zahanati pamoja na kukaa na wataalamu wa taasisi za fedha kuona namna ya kuanzisha Saccos au chombo cha fedha ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa kata hiyo kukopa na kufanikisha maendeleo yao.
Mgombea huyo amewaomba wananchi wa eneo hilo Januari 22, mwaka huu wamchague ili awatumikie baada ya kata hiyo kukosa maendeleo kwa zaidi ya miaka 20.
Uchaguzi huo mdogo wa ngazi ya udiwani unafanyika katika kata hiyo kufuatia aliyekuwa diwani kufariki dunia mapema mwaka jana na nafasi hiyo kuwa wazi.
No comments:
Post a Comment