Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja
na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo
jipya la kituo cha Amani na Usalama
(JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa
nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa
mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama
kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere
katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul
Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya
Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius
Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment