Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga,Mhina Mustapha
Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji
wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka
kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao
kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo
la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na
wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya
kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa
huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa
Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosi
akisisitiza jambo kwa wasafirishaji
hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa
Mbaruku
MBUNGE wa Jimbo la Tanga
(CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimika kuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga
waliotaka kupigwa na
wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madai ya kukamata magari yanayotakiwa
kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.
Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na
kumlazimu Mbunge huyo
kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasi na Emanuel Lyimo ambao walikuwa
tayari wamezingizwa na wafanyabiashara hao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.
Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu
na Assad Hotel ambapo kumekuwa
kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata
moja ya gari linaloelekea
mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.
Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupo mkoani Tanga mapumziko ya mwishoni
mwa wiki kabla ya kwenda mkoani
Dodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la
tukio na kuwachukua askari hao
kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisi zao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.
Akizungumza na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwa watulivu kwani suala hilo
linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzi kutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo
vinatarajiwa kuketi hivi
karibuni mjini hapa.
Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao
kuchukua ushuru bila ya
kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambaye alisema wao wanafanya kazi chini ya
Halmashauri ya Jiji hilo na
wanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari
zote ambazo zinatakiwa kupaki
kwenye stendi kuu ya Kange.
Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo
na atakae kwenda kinyume
atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao
kuonekana kutokuwa na mashine za
kielektroniki.
Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za
Tanga Mombasa Mohammed Nassor
alisema kuwa swala liliwashitua zaidi ni kutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali
ilivyoelekeza jambo ambalo
lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.
Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj
Mustapha Selebosi alisema
halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs na hawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila
kuwepo kwa mashine hizo.
Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari na kulipeleka depo ya Halmashauri
ambao ndio kunafanyika taratibu za
kutozwa faini kwa mfumo wa mashine za
EFDs
No comments:
Post a Comment