Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu
maswali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika leo jijini Mbeya.Kulia
ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kanali Mstaafu Masoud Ally.( Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kapteni
Mstaafu Goerge Mkuchika, akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali
yaliyoelekezwa kwa Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kamati
hiyo imekutana jijini Mbeya kwa ziara ya
kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Juliana Shonza
(katikati) akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali yaliyoelekezwa kwa
Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi .Wengine ni wajumbe wa
kamati hiyo.Kamati hiyo ya Bunge iko
jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu
wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza wakati wa mkutano na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,iliyokutana jijini Mbeya kwa
ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi, Asumsio Achachaa, akijibu
maswali yaliyoelekezwa kwenye Idara yake na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa mkutano na
kamati hiyo iliyokutana Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu
wa Jeshi la Magereza mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi(ACP) Paul Kajida, akijibu maswali yaliyoelekezwa
kwenye Idara yake na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa mkutano na kamati hiyo iliyokutana Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment