Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimpokea Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wapili
kushoto), wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli
zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
Kanali Mstaafu Masoud Ally, akiwaongoza wajumbe wengine wa kamati hiyo
kusalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara ya kikazi ya
kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe,
wilayani Mbalizi, Jijini Mbeya. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiongozana na Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu
Masoud Ally (wakwanza kulia), kuingia ndani ya Gereza la Kilimo la Songwe,lililopo
wilayani Mbalizi, jijini Mbeya, ambapo
wajumbe wa kamati walipata fursa ya kusikiliza maoni kupitia risala iliyoandaliwa na wafungwa wa gereza
hilo.Wengine ni viongozi wa gereza hilo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
Afisa
wa Jeshi la Magereza akijibu maswali
yaliyoulizwa na wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea shamba la
mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo la Songwe, lililopo wilayani
Mbalizi, mkoani Mbeya.Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa
habari baada ya kumaliza ziara ya kutembelea shamba la Mahindi linalomilikiwa
na Gereza la Kilimo Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, jijini Mbeya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment