Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa tatu kulia) akielekea eneo la kufanya usafi
kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo jana jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio
na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho
ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani
akitoa maelekezo ya kufanya usafi kuzunguka ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiendelea kufanya usafi katika
moja ya sehem ya kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo leo jijini Dar es
salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya
kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
Baadhi ya watumishi wakikata matawi ya miti kwa makini bila kuharibu nyaya za
simu yaliyokuwa kizuizi katika barabara eneo la ofisi za Wizara ya Fedha kwa
lengo la kufanya usafi jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wakiendelea kufanya usafi kuzunguka
maeneo ya ofisi za wizara hiyo jana jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji
wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe
za Uhuru mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na watumishi wa wizara hiyo jana jijini
Dar es salaam mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi ikiwa ni mwitikio na
utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe
za Uhuru mwaka huu.
Baadhi ya watumishi
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile(hayupo
pichani) mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi kuzunguka maeneo ya
ofisi za wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
(Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile leo ameiongoza wizara hiyo katika kuitikia na
kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo lao la kazi katika maadhimisho ya sherehe
za Uhuru ya mwaka huu.
Akiongea na watumishi
wa Wizara hiyo, Dkt. Likwelile alisema kuwa maadhimisho ya siku ya uhuru
yaendelee kutumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi ikizingatiwa
dhana iliyokuwepo tangu uhuru ilikuwa “Uhuru na Kazi” ambapo kwa sasa kaulimbiu
ya Rais Dkt. Magufuli inasema “Hapa Kazi Tu”
“Ni uamuzi mzuri wa
Rais, ni wa busara na unaendana na tulipotoka ambapo Tanzania inaamini katika “Uhuru
na Kazi”, huu ni mwanzo wa kusimama kwa miguu yetu wenyewe ili kujiletea
maendeleo kwa kuendelea kuwapiga vita maadui watatu wa taifa” alisema Dkt.
Likwelile.
Dkt. Likwelile
aliwataja maadui hao kuwa ni ujinga, maradhi na umasikini ambao ndiyo wamekuwa
chanzo cha kurudisha nyuma juhudi za maendeleo, kwa kuimarisha suala la usafi
katika mazingira yote nchini, itakuwa mwanzo wa kupambana na suala magonjwa milipuko
ikiwemo kipindupindu ambao asili yake ni uchafu.
Aidha, Dkt. Likwelile
aliwaasa watumishi wa wizara hiyo na Watanzanaia kwa ujumla kuenzi kazi
iliyonzishwa na Mhe. Rais Dkt. Magufuli ya kufanya usafi na zoezi hilo
liwe endelevu na la kudumu ambapo
ameahidi kuwa wizara yake itapanga siku ya kufanya usafi mara kwa mara katika
maeneo ya kazi ili kudumisha usafi ambao ni suala muhimu katika kuimarisha afya
zao na ikizingatiwa watumishi hutumia muda mwingi wakiwa katika maeneo ya kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani alisema
kuwa mwitikio wa watumishi katika zoezi la usafi umekuwa mkubwa na
wanapendekeza zoezi hilo liwe endelevu maana watumishi hutumia muda mwingi
katika maeneo ya kazini hivyo ni vema kuyaweka mazingira hayo katika hali ya
usafi ili yawe rafiki wakati wote wa kutekeleza majukumu yao.
Naye mmoja wa watumishi
wa Wizara hiyo William Muhoja alisema kuwa zoezi la kufanya usafi katika maeneo
ya kazi linatakiwa kufanywa kila wakati
ambapo itakuwa ni sehemu ya watumishi kuwajibika kwa jamii katika maeneo yao
wanapoishi na wanapofanya kazi.
Sherehe za uhuru mwaka
huu nchini zimeadhimishwa kwa namna tofauti na ilivyozoeleka miaka iliyopita
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mamlaka
aliyonayo kikatiba alitangaza maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri ya 9
Disemba mwaka huu, Watanzania wote
waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni,
viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa
vitendo.
Maadhimisho hayo yanaendelea
nchi nzima ambapo kila halmashauri inatekeleza agizo la Mhe. Rais kwa vitendo
kwa kufanya usafi katika maeneo yao, zoezi linashirikisha Wizara, idara,
taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali, maeneo ya viwanda, shule, vyuo,
maeneo ya biashara, masoko na kuzunguka maeneo yote ya makazi ya watu.
No comments:
Post a Comment