Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tanzania (GPFT), Martha Ng'ambi (wa pili kulia), akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dk.Abu Mvungi (kushoto), Dar es Salaam jana asubuhi kabla ya wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho kushiriki kufanya usafi ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuyatumia Maadhimisho ya Siku ya Uhuru 2015 kufanya usafi. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika hilo, Hilda Ngaja.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dk.Abu Mvungi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kufanya usafi maeneo mbalimbali ya chuo hicho.Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tanzania (GPF), Martha Ng'ambi (kulia), akishiriki kufanya usafi.
Usafi ukiendelea chuoni hapo.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiendelea na usafi.
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dk.Abu Mvungi, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi wakati wote badala ya kusubiri kuhimizwa na viongozi.
Dk.Mvungi alitoa mwito huo wakati akilishukuru Shirika la Global Peace Foundation Tanzania (GPF) kwa kuichagua Taasisi hiyo kufanya usafi ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli la kuyatumia Maadhimisho ya Siku ya Uhuru 2015 kufanya usafi.
"Niwapongezi GPF kwa kuunga mkono agizo la Rais la kuja kushirikiana nasi kufanya usafi katika taasisi yetu ambapo wito wangu kwa watanzania kila mmoja wetu awe na utamaduni wa kufanya usafi bila ya kusukumwa na viongozi" alisema Dk. Mvungi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tanzania (GPF), Martha Ng'ambi alisema waliona vema kufanya usafi katika taasisi hiyo kutokana na kuwa na vijana ambao wanafanyakazi nao ili kuwahamasisha katika tukio hilo kubwa la kitaifa.
"GPF ni shirika linalojishughulisha zaidi na vijana ndio maana tuliona ni vizuri kufanya usafi katika taasisi yenu kwa niaba ya vyuo na taasisi zingine ili kuwashirikisha vijana ambao tunafanya nao kazi" alisema Ng'ambi.
Alisema shirika hilo limekuwa likishilikiana na serikali katika masuala mbalimbali licha ya kuwa bado ni changa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment