Watu 19 wakiwemo watalii 17 wa kigeni wameuawa baada ya wapiganaji kulenga jengo moja la kumbukumbu za kihistoria katika mji mkuu wa taifa hilo.
Raia wa Italia, Uhispania na Wajerumani ni miongoni mwa wale waliouawa waziri mkuu Habib Essid amesema.
Washambuliaji wawili pamoja na afisa mmoja wa polisi wameuawa katika oparesheni ya kiusalama iliofanywa, maafisa wanasema. Shambulio hilo lilifanyika katika jengo la kumbukumbu la Bardo Museum ambalo liko jirani na Bunge katikati mwa Tunisia wakati wa shambulio hilo, wabunge walikuwa wakijadiliana kuhusu sheria dhidi ya ugaidi.
Watu wameondolewa katika majengo ya Bunge.
Raia wa Uingereza, Italia, Ufaransa na Uhispania ni miongoni mwa waliotekwa wakati wa shambulizi hilo,kituo kimoja cha redio nchini humo kimetangaza.
Mateka waliosalia katika jumba hilo la kumbukumbu wameachiliwa ,shirika la habari la Reuters limesema baada ya kupata habari hizo kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutajwa.
CREDIT: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment