Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 16 March 2015

WAANDISHI, WANAHARAKATI MBARONI DR CONGO

Lambert Mende waziri wa habari na msemaji wa serikali ya DR Congo.
Waandishi wa habari wa kigeni, wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakiwemo waandishi wa habari wa BBC.

Wanaharakati hao, ambao ni vijana kutoka nchini Burkina Faso, Senegal na Congo, walikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu jukwaa jipya la kijamii.
Mwandishi wa BBC Maud Jullien anaripoti kuwa wanaharakati kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Senegal na Burkina Faso walikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa unaohusu kuundwa kwa jukwaa jipya la kijamii la vijana wa Congo.
Hapo ndipo walipokamatwa na kupelekwa makao ya usalama wa taifa.
Waandishi wa BBC ni miongoni mwa waliokamatwa na wanasema wamewaona polisi wakiwapiga baadhi ya wanaharakati kwa kutumia marungu.
Lambert Mende ambaye ni msemaji wa serikali ya Congo amesema mkutano huo haukuwa halali na kusema kuwa raia waliokamatwa kutoka Senegal na Burkina Faso ni wachochezi hatari kwa usalama wa taifa la Congo.
Nchi ya Burkina Faso na Senegal zote zilikuwa na vuguvugu dhidi ya marais wao walipojaribu kubaki madarakani baada ya muda unaoruhusiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi zao kumalizika.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo atakamilisha muhula wake wa mwisho ifikapo Januari, 2016.
Watu zaidi ya arobaini wameuawa katika vurugu zilizosababishwa na muswada wa uchaguzi ambao ungemuongezea muda wa kukaa madarakani.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment