Katika mechi ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar, Yanga walilala kwa bao 1-0 lililofungwa na Paul Ngwai
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho (Jumatano) kwa viwanja vitatu kutimua vumbi, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Kagera Sugar mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Jijini Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Simba SC katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya wenyeji Mbeya City watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment