Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 24 March 2015

UTT-Amis MKOMBOZI WA WANYONGE TABORA

Displaying _MG_2312.JPG
Afisa masoko mkuu mwandamizi wa taasisi ya UTT-Amis Mfaume Kimario akitoa mada kwenye moja ya semina aliendesha mkoani Tabora hivi karibuni.

Na Hastin Liumba, Tabora
UTT-Amis ni Taasisi ya serikali iliyo chini ya wizara ya fedha ambapo dhumuni kuu ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini ili kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji.



Aidha toka kuanzishwa kwake miaka 12 iliyopita UT-Amis  imeweza kujidhihirisha ni taasisi itakayokuwa mkombozi wa watu wa pato la chini na kati.

Afisa masoko mkuu mwandamizi wa UTT-Amis Mfaume Kimario alifanya mazungumzo na mwandishi wa makala hii kueleza na kufafanua kwa kina nini maana ya Taasisi hiyo na mifuko waliyoanzisha chini ya wizara ya fedha.

Kimario anasema toka wameanzisha UTT-Amis wamekuwa wakitembelea wadau mbalimbali na kutoa elimu na kuhamasisha watanzania kujiunga na mifuko ili kukuza mitaji yao.

Afisa masoko huyo anabainisha taasisi ambazo wamekuwa wakizitembelea ni wafanyakazi wa taasisi za serikali,taasisi zisizo za kiserikali, wafanyabiasha,vyama vya ushirika na vile vyama vikuu vya ushirika kama chama kikuu cha ushirika kanda ya magharibi WETCU ambacho kina vyama vidgogo zaidi 202.

Kimario aliongeza UTT-Amis hadi sasa toka imeanzishwa mifuko hii ina wawekezaji zaidi 100,000 huku kukiwa na thamani ya sh bilioni 235.

Kimario alitaja mifuko waliyoanzisha kwa sasa ni mitano ambayo ni mfuko wa umoja ambao ulianzishwa mwezi Mei 16, 2005 ni mfuko uliolenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji.

Afisa huyo anataja mfuko mwingine ni mfuko wa Wekeza Maisha ambao ulianzishwa mwezi Mei 2007 ni mfuko ulioambatanisha uwekezaji pamoja na faida za bima ambapo mfuko huu unatoa faida ya bima  ya maisha na faida za uwekezaji.

Kimario anataja wahsika wa kuwekeza katika mfuko huu ni mtu yoyote aliye na umri wa miaka 18-55 na muda wa uwekezaji ni kipindi cha miaka kumi (10).

Aidha anaeleza kiasi cha kuwekeza ni sh 1,000,000 ambapo mwekezaji ana uwezo wa kuwekeza kiasi chochote kisichopungua kisichopungua kiasi cha sh 8,340 kila mwezi.

Anaongeza faida kadhaa za mfuko wa Wekeza Maisha ni, bima ya maisha, bima ya ajali, bima ya ulemavu wa kudumu na gharama za maisha.

Aliongeza faida ya uwekezaji kwenye mfuko huu ni ukuzaji wa thamani ya uwekezaji (Vipande) na mkopo wa pongezi baada ya uwekezaji kwa miaka kumi (10).

Afisa huyo alitaja mfuko mwingine kati a mitano ni Mfuko wa Watoto (faraja kwa watoto) alisema mfuko wenye dhumuni la kuwanufaisha watoto wetu kwa ajili ya maisha yao ya badaye na ulianzishwa mwezi Oktoba 2008.

Alisema akiba mapema kwa watoto kwenye sekta ya elimu ni muhimu hasa ikizingatiwa gharama za elimu kwa sasa ambapo ni vyema kuwawekea watoto akiba kwani elimu ufunguo na mwanzo wa maisha ya watoto wetu.

Kimario alibainisha kuna faida mbili kwenye mfuko huu ikiwemo kulipa ada za masomo na mpango huu ni kwa ajili ya malipo ya ada ya masomo ya mtoto mwekezaji.

Aidha faida nyingine ni kukuza mtaji ambapo mpango huu ni kukuza mtaji wa mtoto mwekezaji na umri wa chini ya miaka 18 na gharama za kiasi cha kuwekeza ni sh 10,000 na kuendelea na kiwango cha nyongeza ni sh 5,000.

Alitaja mfuko mwingine ni mfuko wa kujikimu ambao ulianzishwa mwaka Oktoba 2008 ambao ulilenga la kutoa gawio la mara kwa mara huku likilenga kukuza mtaji kwa wale wawekezaji wa muda mrefu.

Kimario anasema kwenye mfuko huu aina mbili za uwekezaji ambazo ni mpango wa gawio na mpango wa kukuza gawio.

Anaeleza mpango wa kukuza gawio ni kwenye mfuko huo ni kila robo ya mwaka mwekezaji atapata gawio kila robo ya mwaka na kila mwaka mwekezaji atapata gawio la mwaka.

Aidha katika mpango wa kukuza mtaji mpango huu ni kwa wale wawekezaji ambao wanaotaka kukuza mtaji wao,hadi siku watakapozihitaji na kiasi cha uwekezaji kwa mpango wa Robo ya mwaka kima cha chini cha kuwekeza ni Sh 2,000,000 tu.

Alisema kwa mpango wa kima cha chini kwa mpango wa mwaka ni kuwekeza milioni 1,000,000,mpango wa kukuza mtaji ni sh 5,000 na uwekezaji wa nyongeza ni sh 15,000 kwa mpango wa gawio na sh 5,000 ni kwa mpango wa kukuza mtaji.

Alitaja mfuko mwingine ni mfuko wa Ukwasi (Ishi vizuri Nastahili) ulionzishwa mwezi Machi 2014 ni mfuko unaokua ambao una nafasi ya uwekezaji kwa watu binafsi,taasisi na vikundi ambao una nafasi ya kuwekeza fedha za ziada.

Alisema kiwango cha chini cha kuwekeza ni Sh 5,000,000 na kiwango cha chini cha nyongeza ni sh milioni 1,000,000 huku kukiwa hakuna kikomo katika kiwango ch juu cha uwekezaji.

Alisema kwenye mfuko huu hakuna ada ya kujiunga wala kujitoa ambapo fedha za mauzo ya mwekezaji za vipande atazipata ndani ya siku tatu za kazi

Kimario aliwaomba wakazi wa Tabora kutumia fursa hiyo hadimu kujiunga na mifuko hiyo yenye sifa na nafuu kwao.

Alitaja mikoa ambayo hadi sasa wamefungua huduma hizo ni jijini Dar-es-Salaaam,jiji la Mbeya,jiji la Arusha,Mkoa wa Dodoma,jijini Mwanza,Zanzibar na sasa mkoani Tabora ambapo mikoa ambayo bado uwepo wa ofisi hautakuwepo wakala wao atayetoa huduma zao ni Benki ya CRDB.

Afisa tawala (Utumishi) mkoa wa Tabora Ali Bushir mara baada ya semina iliyohusisha watumishi wa ofisi yake alikiri mifuko iliyotajawa hapo ni wakati sasa watu kujiunga nayo.

Bushir aliwataka watumishi hao na jamii kwa ujumla kutopoteza fursa hiyo muhimi na adimu kwa kipindi hiki cha sasa.

Nao baadhi ya washiriki wa semina zilizoendeshwa na UTT-Amis waendesha bodaboda chini ya mwenyekiti wao Waziri Kipusi walisema ni mifuko ambao imeangalia gharama zamaisha hivyo kwao ni saizi yao.

hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment