Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 22 March 2015

UMOJA WA MAKANISA TABORA WAUNGA MKONO TCF


Na Hastin Liumba, TaboraUMOJA wa makanisa mkoani Tabora unaoundwa na madhehebu yote ya CCT, TEC na makanisa ya kipentekoste wameunga mkono tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF)  juu ya hali ya usalama wa nchi.


Akitoa tamko hilo kwa niaba ya makanisa Askofu wa kanisa la Kanisa la Anglikana jimbo la Tabora Elias Chakupewa alisema yako mambo manne ambayo yamewasukuma kufanya hivyo ikiwemo uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi.

Askofu Chakupewa alisema kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi kunakiuka misingi ya taifa kwa serikali kutokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia kwa misingi ya dini.

Alisema mjadala unaoendelea unavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Ibara ya 19) kwa kuendelea kujadili hili katika ilani ya vyama vya siasa,majukumu ya kisiasa na bungeni limegawa taifa.

Aliongeza mahakama ya Kadhi imeendelea kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kama mtaji wao kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini na hivyo Tabora nasi tunatamka mjadala unaonendelea kati ya serikali na vikundi vya dini kuhusu mahakama ya Kadhi unafungwa.

Akizungumzia katiba pendekezwa Askofu huyo alisema katiba hiyo inaleta mgawanyiko mkubwa kwa taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiuadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.

Alisema katiba hiyo bado haijajibu matakwa ya malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa serikali,miiko na maadili ya viongozi wa umma.

“Katiba pendekezwa ilipitishwa kwenye bunge la katiba kwa ahadi ya serikali kuipa dini ya kiislamu mahakama ya Kadhi……huku dhahiri rushwa kuchukua nafasi kwa jambo hili.”aliongeza.

Aliomba waumini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,waisome katiba pendekezwa na wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya ‘Hapana’.

Kuhusu usalama wa nchi alisema wanasikitishwa na viashiria vya ugaidi vinavyojitokeza kwa sasa nchini ikiwemo uvamizi vituo vya polisi,uporaji wa silaha,mafunzo ya karate katika nyumba za ibada na mauaji ya viongozi wa dini.

Aidha mauaji ya watu wenye ulemavu ngozi (Albino) umoja wa makanisa Tabora umesikitishwa hali ya mwendelezo wa mauaji ya watu hao huku wengine wakipata vilema vya kudumu.

Alibainisha hali hiyo inatishia hali ya utulivu,amani na umoja wa kitaifa uliopo na wanaasa jamii kuacha kufanya mauaji ya Albino huku hali ya kutoawajika kwa baadhi ya viongozi wa serikali kunaongeza kasi ya mauaji hayo.

Askofu huyo anaeleza kingine ni wigo mkubwa uliopo Kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo vya kikatili na kushangazwa na operesheni kadhaa pale panafanyika ujangili ikiwemo viongozi kuwajibika kwa nafasi zao.

“Tunaomba serikali yetu ikomeshe mauaji ya Albino,ugaidi,uvunjifu wa amani unaoendelea kutokana na mikakati hafifu na udhifu unajitokeza wakati wa kusimamia misingi iliyolea taifa letu.”aliongeza.

Alibainisha hali iliyopo inaonyesha serikali ya CCM imeshindwa kulea misingi ya taifa hili kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani.

Benson Alex alisema anaunga mkono hatuo hiyo kwani taifa kwa sasa limepoteza matumaini kwa watanzania,hivyo semina hiyo itawapa mwanga ni wafanya kwenye kura ya Hapana ama Ndiyo.

No comments:

Post a Comment