Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anayesimamia Kitengo cha Uratibu na Uwezeshaji Dr. Steven Kissui (aliyesimama) akifungua mafunzo ya jinsi ya kujikwamua na umasikini kwa Vijana wa Manispaa ya Singida,Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa aliyesimama akivifundisha vikundi mbalimbali vya vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida mjini namna ya kuandika miradi ya maendeleo,mafunzo hayo yamefanyika Wilayani humo ikiwa ni juhudi za Serikali kuwakwamua vijana katika matatizo yanayowakabili.
Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga akitoa mada ya jinsi ya Mfuko wa Vijana unavyofanya kazi.
Afisa Vijana wa Mkoa wa Mbeya Bw. Masele Lauriani Akitoa mada ya jinsi ya kuwa mjasiriamali katika mafunzo yanayoendeshwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Vijana wa Mkoa wa Singida.
Na Benjamin Sawe, WVUM-Singida
Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo imewaasa vijana wa kikundi cha Mapambano Vijana Saccoss kuzingatia
vigezo wanapoomba mikopo katika mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo anayesimamia Kitengo cha Uratibu
na Uwezeshaji Dr. Steveni Kissui alipotembelea Ofisi ya Mapambno Vijana Saccoss Ltd iliyopo
Manispaa ya Singida mjini.
“Vikundi vya vijana wanaoomba mkopo katika Mfuko wa Vijana ni
vyema wakazingata vigezo vinavyotakiwa kufuatiliwa pale wanapoomba mikopo kwani
muongozo upo wazi na unaelekeza vizuri hivyo kwa kufanya hivyo suala la kupata
mkopo kwa wakati kupitia mfuko huo utakuwa rahisi, kwa mfano kigezo cha umri ni
muhimu kuzingatiwa ikibainisha umri wa kijana ni kuanzia miaka 15 hadi 35”
Alisema Bw. Kissui.
Naye Mwenyekiti wa Mapambano Vijana Saccos Bi. Halima Sadiki amewashauri
vijana wenzake kuacha kulalamika badala yake wajiunge na kuanzisha vikundi ili
kuweza kupata mkopo na kuweza kujitatulia matatizo yao.
“Tunaushukuru sana uongozi wa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na
Michezo, kwa kutuma viongozi wake kututembelea hapa Manispaa ya Singida na
kutupatia elimu juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, ikiwemo mambo ya
kuzingatia tunapounda vikundi vya vijana”,alisema Bi Halima.
Hata hivyo serikali imewashauri vijana hao kuandika mradi na
kuainisha mchanganuo wake vizuri pale watakapo omba mkopo na kuzingatia mambo
yote muhimu yaliyopo katika mwongozo kwani serikali imedhamiria kuwakomboa
vijana kwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Wakati huohuo Dr. Kissui alisema
kumekuwa na dhana miongoni mwa Vijana kuwa Serikali ndio mwajiri Mkuu na
kusahau kuwa ujasiriamali ndio suluhisho
pekee la tatizo la ajira kwa Vijana.
“Vijana mnatakiwa kujiunga ikiwa ni pamoja na
kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali na kuacha tabia ya
kulalamika.Alisema Dr. Kissui
No comments:
Post a Comment