Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 13 March 2015

SAKAYA APANGA KUMNG`OA KAPUYA


Na  Hastin Liumba,Usinge

MBUNGE wa viti maalumu chama cha wananchi (CUF) Magdalena Sakaya amesema atachukua fomu kugombea jimbo la Urambo Magharibi wilayani Kaliua mkoa wa Tabora.


Kauli hiyo aliitoa kwenye mkutano wa hadhara wakati akiongea na wananchi wa kata ya Usinge wilayani Kaliua.

Sakaya alisema kikubwa kinachomsukuma kugombea ubunge wa jimbo hilo kunatokana na hali mbaya kiuchumi na huduma za kijamii ambazo kimsingi anaona wananchi wametelekezwa.

Aidha kingine kilichomsukuma ni unyanyasaji unaofanywa kwa wananchi jamii ya wafugaji na kusema baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia wafugaji kama mtaji wao huku wakiwatukana wafugaji kuwa ni ‘Manyani’.

Alisema licha ya hayo bado huduma za maji na afya ni mbovu kwa kiasi kikubwa na zaidi kinamama wajawazito wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa huduma nzuri za afya ikiwemo upungufu wa watalaamu wa afya.

Sakaya alisema kwa wilaya ya Kaliua kuna zahanati na vituo vya afya 34 na watalamu wa afya wako 44 tu hali ambayo inatia uchungu na zaidi kina mama wajawazito wamekuwa wakitamka wakifikia hatua ya kujifungua wanapata mawazo kwa kukosa huduma.

Alisema kingine ni hali mbaya waliyonayo wakulima hasa wa tumbaku na kuongeza wengi wao hadi sasa hawajalipwa malipo yao na kufikia hatua mabenki wameshindwa kuwakopesha kwa kukosa sifa.

Mbunge huyo anasema licha matatizo hayo bado kumekuwa na viongozi ambao wanawagawa wananchi kwa ukabila na udini.

Alisema kiwango cha kugawa wananchi kwa ukabila na udini kimekuwa kwa kiasi kikubwa na kuahidi endapo atapata nafasi ya kuwa mbunge ataondoa dhana hiyo ikiwemo kutatua kero zinazokabili wananchi wa jimbo hilo.

“Ndugu zangu mimi ni mwanamke lakini pamoja na hilo siogopi vitisho vyovyote vile wala siogopi hata nguvu za giza kwani jimbo la Kaliua siyo la mtu binafsi…..nitagombea na nitashinda tu.’alisema.

Alisema wananchi mmenyanyasika kwa muda mrefu hivyo muda wa kuifuta CCM madarakani umefika na silaha ya kuiondoa ni kwenda kujiandikisha muda ukifika ili shetani CCM ang`oke.

Aidha Sakaya alisema hali ya kiuchumi ni mbaya kwani tunategemea wahisani kutekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 70 na hili ni hatari kwa ustawi wa nchi na wananchi wake.

No comments:

Post a Comment